Tume ya Ushirika yawatahadharisha viongozi AMCOS

0
151

Derick Milton, Simiyu

KAMATI ya udhibiti na usimamizi tume ya Maendeleo ya Ushirika amewataka viongozi wa Amcos kuachana na tabia ya kula pesa za chama na kuziona kama sumu kwani hawataonewa huruma bali watakumbana na kesi za uhujumu uchumi.

Kamati hiyo ikiongozwa na Robert Busuma na Mudhihir Mudhihir ambao wote ni makamishna wa tume hiyo wamesema hayo leo, wakati wa ziara yao mkoani Simiyu ya kutembelea vyama vikuu na vya msingi vya ushirika.

Wakiwa katika chama cha msingi cha Zuya, makamishna hao wamewataka viongozi kuachana na tabia za ubadhilifu wa mali yeyote ya chama bali wahakikishe wanawatumikia wanachama.

“ Niwatake viongozi wa Amcos kuziona mali za chama, pesa za chama kama sumu, mzione kama moto, acheni kabisa, tutawachukulia hatua kali zaidi, ukiwa kiongozi wa ushirika watumikie wanachama na siyo kula pesa za chama,” alisema Busuma.

Wakiwa kwenye chama kikuu cha ushirika (SIMCU) makamishina hao wamekipongeza chama hicho kwa kazi nzuri ikiwemo kusaidia watu wenye mahitaji maalumu pamoja na kushirika katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

“ Kazi ambayo imefanywa na SIMCU kushiriki shughuli za maendeleo, kusaidia wenye ulemavu, ndiyo tafsiri sahihi ya ushirika toka zamani, mna kazi kubwa ya kuhakikisha chama hiki kinawasaidia wakulima,” amesema Mudhihiri Mudhihir.

Naye Mrajisi wa Mkoa Ibrahimu Kadudu amesema wameendelea kuwachukulia hatua viongozi wote ambao wamekuwa wakihusika na wizi katika vyama, ambapo kwa mwaka huu jumla ya kesi nne za uhujumu uchumi zimefunguliwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here