27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Tume ya uchunguzi sakata la wizi mashine ya ultrasound Simiyu yaanza kazi

Derick Milton, Simiyu  

Hatimaye tume iliyoundwa kuchunguza sakata la wizi wa mashine ya ultrasound katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu imeanza kazi.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Jumatano Agosti 21, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini amesema  wametekeleza maagizo na tayari tume hiyo imeanza kazi jana ambapo inatakiwa kukamilisha kazi hiyo na kukabidhi Agosti 23, mwaka huu.

“Taarifa yao itaainisha chanzo cha wizi huo, nani wahusika, kama ni uzembe, na watakuja na mapendekezo ya nini kifanyike, njia ya kurudisha mashine hiyo, lakini pia watakuja na mapendekezo ya nini kifanyike kuzuia wizi usitokee tena kwenye hospitali hiyo,” amesema Sagini.

Amesema licha ya kuundwa kwa tume hiyo, bado vyombo mbalimbali vya kiuchunguzi vya serikali vinaendelea na kazi yake ya kuhakikisha wanampata mhusika au kupatikana kwa mashine hiyo.

Mashine hiyo iliibwa hospitalini hapo Agosti 3, mwaka huu ambapo Mkuu wa Wilaya ya Simiyu, Festo Kiswaga aliagiza watumishi 137 wa hospitali hiyo kuchanga fedha kulingana na mishahara yao kufidia mashine hiyo.

Hata hivyo, agizo lilitenguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Suleiman Jafo akiagiza kuundwa kwa tume ya uchunguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles