Na ANDREW MSECHU-DAR ES SALAAM
MKURUGENZI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Athuman Kihamia amemtaka Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amuombe radhi ndani ya siku saba la sivyo atamshtaki kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kihamia alisema tuhuma dhidi ya ofisi yake zilizotolewa na Mbowe juzi kuhusu kuongeza vituo na maofisa wa tume kuwazuia mawakala wake ni za uongo na hazina ushahidi.
Alisema kwa kuwa ametajwa yeye kuwa ndiye aliyeandaa mpango wa kuongeza vituo hivyo, suala ambalo si kweli, ni vema kiongozi huyo wa Chadema, achukue hatua za sheria kwa kwenda mahakamani na si kumchafulia jina lake.
“Kwa mambo hayo ya kihuni anayoyafanya Mbowe anatakiwa akome kuanzia hiyo juzi. Iwe mara ya mwisho.
“Kama kuna kasoro yoyote afuate utaratibu. Anajua kuna kamati za maadili, kuna kamati za rufaa na kuna mahakama,” alisema.
Alisema ameamua kuzungumza na wanahabari kuhusu hilo baada ya kuona kiongozi mkubwa kama Mbowe anafanya mambo ya uhuni huku akijua kwamba tume ni taasisi inayofanya kazi zake kwa mujibu wa sheria.
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.