Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kikaangoni

0
684

Na Mwandishi wetu-Dodoma

WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga ameipa wiki moja Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kutengeneza mikakati ya kutengeneza mabwawa ya kukinga maji ya mvua ili kuwasaidia wakulima kukuza kilimo cha umwagiliaji.

Hasunga alisema hayo juzi katika ukumbi wa ofisi ndogo za Wizara ya kilimo Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza kwenye kikao kazi na watumishi wa tume hiyo. 

Alisema wizara inatarajia kutumia fursa ya mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (RHPP) kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Hasunga aliwataka watendaji wa tume hiyo kuhakikisha wanampatia mipango na mkakati wa namna gani maji ya mradi huo wa umeme, yatakavyoweza pia kutumika kwenye kilimo cha umwagiliaji.

‘’Ninawapa wiki moja hakuna muda mwingine wa kufanya hivyo kwa sababu niliwapa mienzi minne hamjafanya hivyo,’’ alisema Hasunga.

Pia alitoa siku tatu tume hiyo impe taarifa za utendaji kazi wa miradi ya umwagiliaji katika minne ya Tabora, Katavi, Rukwa na Songwe iwapo kuna miradi inayofanya kazi na isiyofanya kazi.  Kilimo cha umwagiliaji kimekuwa kikisisitizwa na Serikali kwani ni kilimo kisichotegemea mvua hivyo kuwa na matarajio ya kuvuna mazao kwa wingi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here