27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Tume ya Mufti Zubery yaomba ushirikiano

Sheikh Aboubakar Zubery.
Sheikh Aboubakar Zubery.

Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

TUME iliyoundwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Aboubakar Zubery, kuhakiki mali za waislamu nchini imewataka waumini wa dini hiyo kutoa taarifa za mali zilizouzwa kihalali au isivyo halali ili waweze kuzihakiki.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo, Sheikh Issa Othman Issa, alisema tume hiyo ni huru na ina wataalamu tofauti  wakiwamo wa kutoka serikalini ambapo lengo lake ni kuhakikisha mali hizo zinapatikana na kurudishwa kwenye mikono ya Waislamu wenyewe.

Alisema ushirikiano wao utaisaidia tume hiyo kufanya kazi zake na kumaliza kwa wakati ili ziweze kuingizwa kwenye kumbukumbu.

Sheikh Issa alisema mpaka sasa tume hiyo imetimiza siku 30 tangu ilipoundwa na itazunguka  nchi nzima ili kufuatilia mali za Waislamu ziweze kurudishwa.

“Tunawaomba waislamu kutoa ushirikiano kwa tume yetu pindi wanapopita kwenye maeneo yao ili tuweze kuingiza kwenye kumbukumbu zetu, jambo ambalo linaweza kurahisisha shughuli hii.

“Ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, tume hiyo imeweza kupita katika maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kufuatilia jambo hilo, hali inayoonyesha wazi kuwa, kazi hiyo ni rahisi na kwamba inaweza kuisha katika kipindi cha muda uliopangwa wa siku 90,” alisema Issa.

Miongoni mwa mambo ambayo yanafuatiliwa na tume hiyo ni pamoja na mikataba ya uuzaji wa viwanja na mali nyingine ambazo zinamilikiwa na Baraza au taasisi zake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles