27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 17, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

TUICO yawataka wanachama kuchagua viongozi watakaolinda maslahi ya Chama

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

CHAMA Cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) kimewataka wanachama wake kujipanga vizuri kwa ajili ya uchaguzi wa chama hicho, ili kuchagua viongozi watakaolinda maslahi na uhai wa chama.

Akizungumza leo, Februari 10, 2025, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa TUICO, Paul Sangeze, wakati wa hafla ya kutia saini mkataba wa hali bora kati ya TUICO na waajiri, amesema wanachama wanapaswa kuhakikisha kuwa viongozi wanaopatikana ni wale wenye maono ya kuimarisha chama.

“Mwaka huu ni wa uchaguzi wa TUICO. Hakikisheni mnapata viongozi bora. Uchaguzi usiwe wa kupitisha wagombea bila kupingwa, hata kama mgombea ni mmoja, kura za ‘Ndiyo’ au ‘Hapana’ ni muhimu,” alisema Sangeze.

Aidha, alieleza kuwa katika mwaka mmoja uliopita, chama kimefanikiwa kuongeza wanachama 15,032, kufunga mikataba 98 ya hali bora, na kushinda migogoro 214 kati ya 303 iliyopokelewa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Sekta ya Biashara TUICO, Willy Kibona, alisema mkataba uliosainiwa utaimarisha maslahi ya wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na waajiri kugharamia matibabu na misaada kwa wafanyakazi wanaopata madhara kazini.

Naye Katibu Msaidizi wa TUICO Kigamboni, Hamisa Simba, alisisitiza mshikamano wa wafanyakazi, akisema mkataba huo uwe chachu ya kuongeza tija na ufanisi mahali pa kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
595,000SubscribersSubscribe

Latest Articles