25.9 C
Dar es Salaam
Saturday, December 3, 2022

Contact us: [email protected]

TUFANYE TATHIMINI YA MANUNUZI YETU

Na Shermarx Ngahemera

MALIPO ya mwisho kwa mzabuni ni muhimu sana katika kuhitimisha muamala wa manunuzi ya jambo lolote ikiwa kama huduma au bidhaa na hivyo yafanyike baada ya taasisi nunuzi kujiridhisha kuwa huduma au kazi imekamilika na kukidhi matakwa ya mkataba.  Ni muhimu kwani baada ya hapo mtoa huduma huchukulia kuwa ni kero na ubabaishaji kwa upande wa mnunuzi.

Hali huwa hicvyo kwa sababu hatua hii itafanyika baada ya mtoa huduma au mkandarasi kuwasilisha maombi ya malipo yake na mnunuzi  kuyapitia na  kuyatathimini vilivyo.

Kuna shughuli nyingi za mahusiano  za kuzingatia kwani  masuala ya fedha na mali huzalisha mambo mengi mtambuka katika usimamizi wa mikataba ya ununuzi wa umma na hivyo yangezingatiwa na wahusika wote ili kufanya mambo yawe muruwa.

Ili kuwa na Mikataba yenye ufanisi ni ile inayojali pamoja na mambo mengine uhusiano wa mtoa huduma na mpokea huduma, ni muhimu kutambua kuwa msingi wa kuendeleza mahusiano kwa pande hizi mbili ni kuwqa na imani  na  kuleta uwazi na mawazo endelevu,  kwa kutatua migogoro katika utekelezaji wa mikataba na kuibua fursa za kuboresha kwa siku za usoni. Mahusiano lazima yatazamwe kwa jicho la kitaalamu na lenye nia pana zaidi hivyo hatua za kitaalamu zitumike kwenye usimamizi na kutatua migogoro ya kimkataba na siyo vinginevyo.

Viasharia hatarishi ni matokeo ya mambo ambayo hayajapangwa au kutabirika, ambapo yakitokea yanaweza kuzuia utekelezaji wa jambo lililopangwa. Hivyo basi, usimamizi wa viashiria hatarishi ni sharti uwe timilifu kwa kuzingatia hali halisi iliyojitokeza au  kuendelea kuwepo ili kufanikisha jambo au mkataba.

Katika mikataba mikubwa  kama ya ujenzi ni  bora kufanya Mapitio ya utekelezaji wa mkataba kwani ni kitendo cha kulinganisha utendaji kazi wa kifaa, kandarasi au huduma kulingana na vigezo vilivyowekwa na kukubalika kwenye mkataba husika. Mara nyingi eneo hili husahaulika hasa baada ya mkataba kukamilika, na wakati mwingine taasisi inaweza ikaingia mkataba mwingine bila kupitia hatua hii. Kuna umuhimu kufanyika hayo kwani yanaweza kutolewa vyeti au maandiko yanayoweza kumsaidia mtoa huduma  kama ithibati ya ufanyakazi  na hivyo  kumsaidia kusitawisha biashara yake na hivyo kuwa na mahusiano mazuri ya mkataba wa manunuzi na utoaji huduma.

Vilevile Utekelezaji wa hatua hii  muhimu utasaidia kujifunza na kutambua makosa na kufanya marekebisho kwa miradi ya baadae ambayo inafanana na miradi iliyokwishatekelezwa. Kimsingi miradi mingi sio mipya bali hujirudia rudia ila kinachobadilika ni sehemu husika  na hivyo ni vizuri tathimini zikafanyika ili  kubaini mapema kilichojificha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,538FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles