22.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Tufanye haya ili kuendelea kuimarisha uwekezaji na ukuaji wa uchumi Tanzania

Tunaelekea kuufunga mwaka wa 2020 na panapo majaliwa itakuwa heri kwetu kuuona mwaka 2021. Miezi hii ya mwisho wa mwaka huwa ni wakati mzuri wa tafakari ya wapi tumefanikiwa mwaka huu.

Kama nchi, Tanzania ina mambo mengi ya kujivunia mwaka huu na mojawapo ni lile la kuingia katika kundi la nchi zenye uchumi wa kati, ikiwa ni miaka mitano kabla ya muda ambao serikali ilikuwa imekadiria.

Mafanikio hayo ya kuingia uchumi wa kati ni matokeo ya uwekezaji wa miaka mingi kutoka kwa serikali na sekta binafsi, lakini pia ni matokeo ya Tanzania kuendelea kuwa sehemu ya kuvutia kwa wawekezaji.

Mwaka huu kwa mfano, Shirika la Fedha Duniani (IMF) limeweka bayana namna mbalimbali ambazo Tanzania imekuwa ikifanya kuvutia wawekezaji katika miaka ya karibuni. Mojawapo ya njia tajwa ni sera bora za kifedha na mitaji.

Shirika hilo limeendelea kuanisha kuwa, katika kuendelea mbele zaidi, zipo namna mbalimbali ambazo Tanzania inaweza kufanya kuongeza ukuaji zaidi wa uchumi wake ili nchi na watu wake kuendelea kunufaika zaidi na zaidi. Eneo mojawapo ambalo limetajwa kuongeza tija iwapo maboresho zaidi yatafanjwa ni mfumo bora zaidi wa kodi na vibali vya kufanya biashara nchini.

Mapendekezo mengine ni kuongeza motisha na mbinu za kuvutia wawekezaji zaidi kuja Tanzania na wakati huo huo kukuza uwezo wa Watanzania wenyewe kutumia fursa za ajira na biashara zitokanazo na wawekezaji hao.

IMF imeendelea kusema kuwa majadiliano ya mara kwa mara kati ya wadau wa uwekezaji toka serikalini na sekta binafsi ni muhimu katika kuhakikisha mapendekezo haya toka pande zote mbili yanafanyiwa kazi.

Hatua muhimu za namna hii zitasaidia kuipa Tanzania faida zaidi na nafasi kubwa ya kuvutia wawekezaji wengi bora ili kuendelea kukuza uchumi wake na watu wake katika sekta mbalimbali mfano mawasiliano ya simu na nishati mbadala. Katika siku zijazo itakuwa muhimu kwa wadau wote kuendelea kukaa pamoja na kusikilizana ili kuwa na mwongozo bora wa kiutendaji na utekelezaji wa pamoja.

Katika kufanya hayo tutakuwa tumeweka msingi wa mazingira ya kufanya biashara, msingi ambao utasaidia uwekezaji wa biashara nyingi kwa miaka mingi ijayo. Mwaka huu tumefanikiwa na ni jambo jema kwamba tumepiga hatua, tuendelee kuwa na matumaini kwamba miaka ijayo itakuwa bora zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,429FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles