32.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 12, 2024

Contact us: [email protected]

TUCTA YACHOKONOA ‘DUDE’ VYETI FEKI

Na JOHANES RESPICHIUS
-DAR ES SALAAM

SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), limeingilia kati sakata la vyeti feki kwa watumishi wa umma kwa kuiomba Serikali iwalipe mafao yao.

Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokya, katika ufunguzi wa kikao cha Bodi ya Wadhamini wa shirikisho hilo.
“Tunawaomba watumishi wote ambao wamepitiwa na kadhia ya vyeti feki wawe watulivu wakati tukiwa tunaendelea kuangalia namna ya kukutana na Rais Dk. John Magufuli, kumweleza changamoto hiyo. Kuna watu wamefanya kazi kwa miaka 40 na walifanya vizuri, hivyo kuwafukuza ghafla tu si haki.

“Kwa sababu waliitumikia nchi kwa weledi na uaminifu na mali za umma zikabaki salama, tunaiomba Serikali iwaangalie kwa jicho la huruma walau wapate hata fedha zao za pensheni,” alisema Nyamhokya.

Katika hataua nyingine, Tucta imewataka maofisa utumishi nchini kuacha kuwaandikia barua za kuwafukuza kazi watumishi wenye elimu ya darasa la saba kwani Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk. Laurean Ndumbaro, alishaagiza wasifukuzwe.
Alisema kuwa wamepata malalamiko kwa wanachama wao ambao wameandikiwa barua za kuachishwa kazi, licha ya kutokuwa na agizo lolote kutoka kwa Katibu Mkuu Utumishi.

“Rais Magufuli akiwa katika sherehe za Mei Mosi, mwaka huu zilizofanyika Moshi, alisema kama mfanyakazi ana cheti cha darasa la saba, hakuna haja ya kudanganya kwa sababu kuna kazi ambazo anaweza kuzifanya kulingana na elimu yake, kwa hiyo maofisa utumishi kuwaandikia barua za kuwaachisha kazi hawana mamlaka hayo kwani hawajapewa agizo la kufanya hivyo,” alisema Nyamhokya.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Tucta, Dk. Yahya Msigwa, alisema hadi sasa shirikisho hilo limeshapokea malalamiko kutoka kwa zaidi ya wafanyakazi 3,000 nchini ambao wametakiwa kuacha kazi.

Alisema watumishi hao wanatoka katika sekta ya afya na elimu na kwamba katika kila hospitali ya mkoa zaidi ya wauguzi 100 wametakiwa kuacha kazi kwa kigezo cha kuwa na elimu ya darasa la saba.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Naunga mkono uamuz huo wa shrkisho la wafanyakaz kuhakikisha wa2mixh waliofukuzwa kaz wanapewa walau kiinua mgongo chao kwa ile miaka waliyoweza kui2mikia xerkal kwan walifanya kaz yao kwa uangalfu halafu leo wanafukuzwa bila kupewa chochote.Tujiulize kwa kpnd hcho maendeleo yalyokuwa yakipatikana yalikuwa yanaletwa na akina nan? Kana cyo hayo wanaoitwa wenye vyet fek tena ndo waliokuwa wanafanya kaz kwlkwl ndo maendeleo 2liyonayo xaxa ambayo 2najivunia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles