25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

TUCTA watoa angalizo mafao kwa wastaafu

 Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolas Mgaya
Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolas Mgaya

Patricia Kimelemeta-DAR ES SALAAM

SHIRIKISHO la Vyama Vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) limeitaka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuhakikisha kuwa, wanalipa mafao ya wastaafu kwa wakati ili kuondoa malalamiko yanayojitokeza.

Akizungumza na MTANZANIA jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolas Mgaya alisema kumekuwa na malalamiko ya uchelewashaji wa mafao hayo jambo ambalo limechangia idadi kubwa ya wastaafu kuishi katika mazingira magumu.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa Shirikisho hilo limewaandikia barua Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), ili kushughulikia tatizo hilo ambalo linaweza kusababisha wafanyakazi kutokuwa na imani nao.

“Tumepata malalamiko kutoka kwa wastaafu ya kuchelewa kulipwa mafao yao hadi zaidi ya mwaka mmoja, jambo ambalo limewafanya wengi wao kuishi katika mazingira magumu,” alisema Mgaya.

Licha ya juhudi hizo Mgaya alisema watakutana na viongozi wa mifuko hiyo ili kuhakikisha kuwa suala hilo linashughulikiwa mapema na kuondoa usumbufu kwa wastaafu.

“Mtu amechangia zaidi ya miaka 40, halafu unachelewa mafao yake unafikiri atakuwa na imani na wewe, lazima ili suala liangaliwe kwa umakini mkubwa kwa sababu linaweza kusababisha wafanyakazi kujitoa kwenye mfuko,”alisema.

Alisema Serikali inapaswa kuwaeleza wafanyakazi kama kuna tatizo la fedha ili waweze kujua kuliko kuwazungusha wakati wa kufuatilia mafao yao, jambo ambalo linaleta usumbufu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles