28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

TUCTA, CCM wazidi kufurahia kikokotoo

FERDNANDA  MBAMILA Na SHA BANDAR ES  SALAAM

NAIBU  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya  Tanzania (TUCTA),  Dk. Yahaya Msigwa  amesema kauli ya Rais Dk. John Magufuli kutengua kanuni ya mafao ya wastaafu (kikokotoo kipya) imeleta manufaa kwa wafanyakazi baada ya kuongezewa muda.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam kuhusiana na sheria hiyo,  Dk Yahaya  alisema alimshukuru Rais kwa  kuiweka kanuni hiyo wazi  kwa wafanyakazi ambayo itapitiwa upya mwaka  2023.

“Rais  ameweka kanuni hiyo ili  kuwapisha wadau  mbalimbali nchini  waje na sheria yenye tija  na inayolinda maslahi ya wafanyakazi kupitia mifuko ya jamii.

Dk Msigwa aliongeza kuwa  awali  mifuko hiyo  ilikuwa mitano lakini hivi sasa miwili baada ya kubadilishwa kwa sheria hiyo hivyo kwa namna moja imewarahisishia wadau kuondoa mkanganyiko ambao uliwaweka gizani,”alisema Dk. Msigwa.

Aliitaja mifuko hiyo ya jamii kuwa ni NSSF ambayo inahusika na sekta binafsi pamoja na PSSSF ambao  niwa watumishi wa serikali.

Wakati huo huo Umoja wa Wazazi Tanzania (CCM), umempongeza Rais Magufuli kutokana na busara ya kurudisha imani kwa wastaafu ambao walikuwa wameipoteza baada ya uamuzi wa serikali kubadili kanuni ya kikokotoo kilichotumiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi, Dk.Edmund Mndolwa  alisema mfumo uliokuwa umepitishwa na serikali wa asilimia 25 ulileta shida kwa wastaafu.

“Jambo hili lilileta sintofahamu ya stahili za wastaafu hao ambapo kulizuka mjadala mkubwa  nchini, Umoja wa Wazazi tunampongeza kwa kuahirisha mchakato huo mpaka 2023 ili wadau wa mifuko hiyo waweze kujadiliana kwa kina kwa faida ya pande zote mbili yaani mifuko ya jamii na wastaafu,”

“Kuendelea kuwa Tanzania ya maadili mema ,utawala bora nchini na naamini nchi itasonga mbele kukiwa na mshikamano,” alisema Dk.Mndolwa.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles