23.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

TTCL YAWAKUMBUKA WATOTO PASAKA

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya TTCL, Nicodemus Mushi

Na MWANDISHI WETU- DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya simu ya TTCL   imekabidhi msaada wa vyakula na vinywaji vyenye thamani ya Sh milioni nne kwa vituo viwili vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu  vilivyopo jijini Dar es Salaam, kusherehekea sikukuu ya Pasaka.

Akizungumza wakati wa kukabidhi  zawadi hizo, Meneja Uhusiano wa Kampuni ya TTCL, Nicodemus Mushi, alisema lengo la kukabidhi zawadi hizo ni kuhakikisha watoto wanaoishi katika vituo hivyo wanafurahia kama ilivyo kwa watoto wengine.

“Huu ni utaratibu wetu wa kawaida tunaufanya katika sikukuu zote, lengo ni kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kuhakikisha wanafurahia siku hii muhimu,” alisema Mushi.

Alisema zawadi zinazotolewa na kampuni hiyo ni sehemu ya kurudisha faida kwa jamii kama ilivyo kwa kampuni nyingine za Serikali, lengo likiwa ni kuwasaidia Watanzania hasa wenye kipato cha chini.

Akipokea msaada huo mwakilishi wa kituo cha Valentino kilichopo Buza jijini Dar es Salaam, Sista Lucy Lisenga, alisema zawadi hizo zitawasaidia watoto hao katika siku za sikukuu kwa kuwa   maandalizi ya kituo yalikuwa hayajajitosheleza.

“Nimeguswa sana, namshukuru Mungu, kutoa ni moyo si utajiri nawashukuru sana TTCL hatujawahi hata siku moja kupatiwa msaada na kampuni hii lakini leo tumepata, naomba na kampuni nyingine ziwe na moyo wa kujitoa kama hawa,” alisema Sista Lucy.

Mmoja wa wasichana wanaolelewa katika kituo hicho, Diana Mosses, aliishukuru kampuni hiyo na kuwaomba wadau mbalimbali kutoa misaada hasa ya vifaa vya shule ambavyo vinawapa shida kuvipata.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,319FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles