24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TTCL yapongezwa kwa hatua kubwa ya utoaji huduma

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

Jamii imeshauriwa kuzingatia maadili ili kuwa na uzalendo katika kulinda na kutunza rasilimali za Taifa ikiwemo miundo mbinu ya mawasiliano.

Akizungumza katika maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima maarufu kama Nanenane, Afisa Mkufunzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Dodoma, Faustine Malecha wakati alipotembelea banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ambapo amesema mawasiliano ndio kiunganishi kikubwa cha usalama.

Amesema analipongeza shirika hilo la mawasiliano kwa hatua kubwa lililochukua katika kuhakikisha linarejea na kutoa huduma za mawasiliano kwa wananchi wake.

“Mtazamo niliokuwa nao kuhusu TTCL na baada ya kufika bandani hapo na kupokelewa na maafisa waliotumia utaalam wao kuelezea shughuli kubwa zinazofanywa na shirika hili nimebaini kuwa maendeleo makubwa yamefikiwa ikilinganishwa na lilivyokuwa hapo awali,” amesema Malecha.

Amesema TTCL ni mpya ambayo kwa sasa imejipambanua katika kutoa huduma za kisasa kulingana na maendeleo ya teknolojia.

Ameongeza kuwa kwa sasa TTCL inatoa huduma bora na kwa haraka ambayo inawezeshwa na faiba inayowawezesha watumiaji wa teknolojia ya mawasiliano kupata huduma kwa viwango vya juu.

“Nimefurahishwa sana na jinsi huduma zilivyopanuka kutoka zilivyokuwa maana sasa TTCL inasikika na huduma zinawafikia watu wengi zaidi,” amesema Malecha.

Ameongeza kuwa TTCL ni chombo kinachotegemewa na Serikali kutokana na umuhimu wake nakwamba imeaminiwa na kupewa jukumu la kusimamia miundombinu ya mawasiliano ikiwemo Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) pamoja na Kituo cha kutunza kumbukumbu (NIDC).

Amesema ni vyema kwa watendaji wa shirika hilo kuhakikisha wanafanya majukumu yao kwakuzingatia weledi, uadilifu na kuwa wazalendo kwa taifa lao huku wakizingatia kuwa chombo hicho wanachokisimamia ni muhimu sana katika kulinda usalama wa taifa lao.

Ameongeza kuwa teknolojia ya kuwafikishia wateja huduma ya mawasiliano kwa njia ya faiba mpaka majumbani na ofisini ni huduma inayohitaji watumishi waadilifu na wanaojituma na kulipongeza shirika hilo kuwa na watu wa aina hiyo ambao wamewezesha huduma hiyo kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Maadhimisho ya Siku Kuu ya Wakulima huadhimishwa Agosti 8, ya kila mwaka ambapo hutanguliwa Na shuhuli mbalimbali zikiwemo za kilimo,uvuvi,ufugaji

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles