28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

TTCL yafurahia ushiriki Wiki ya Huduma za Fedha

Na Mwandishi wetu Arusha

Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL), kupitia kampuni yake  tanzu ya T-PESA, imesema kuwa uwepo wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa  yameongeza chachu katika utoaji wa elimu kwa wateja wake  na wananchi wote kuhusu huduma mbalimbali wanazotoa.

Hayo yameelezwa leo Novemba 24, 2023 jijini Arusha na Ofisa Uhusiano wa TTCL , Adeline Berchimance katika maadhimisho hayo yanayofanyika katika viwanja vya Shekhe Amri Abeid.

Amesema maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na kuzishirikisha taasisi ndogo za fedha, mabenki, mifuko ya hifadhi za jamii na wajasiriamali, yameisaidia  hampuni hiyo kukutana na wananchi na kuwajengea uelewa kuhusu matumizi sahihi ya fedha mtandao na fursa mbalimbali zinazopatikana katika kampuni hiyo zinazoweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.

 “Katika kuunga juhudi za serikali za kutatua changamoto ya ajira kwa vijana T-Pesa inayofursa mbalimbali kwa vijana zinazoweza kuwasaidia kujitengenezea kipato na hivyo kujikwamua kiuchumi.

“T-Pesa inazo fursa ikiwa ni pamoja na uwakala ambapo wanaweza kufanya biashara hii ya kuwa wakala na kujipatia kipato cha kusaidia familia zao kwani tunatoa kamisheni kubwa zaidi ukilinganisha na mitandao mingine,” amesema  Adeline.

Aidha amesema Maadhimisho hayo pamoja na mambo mengine yametoa fursa kwa kampuni hiyo kujibu hoja, maswali na kero z wananchi  na kupata mrejesho sahihi kuhusu huduma na bidhaa  wanazotoa.

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanafanyika kwa mara ya tatu, mwaka huu yakiwa na kaulimbiu, Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Uchumi ambapo Waziri Mkuu wa Kassim Majaliwa, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles