25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Tshishimbi afunguka mbinu iliyowamaliza Lipuli

Theresia Gasper – Dar es Salaam

NAHODHA wa Yanga, Papy Tshishimbi, amesema mipango yao ilikuwa lazima wapate mabao kipindi cha kwanza katika mchezo wao wa juzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Lipuli.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga ilishinda mabao 2-1 na kufikisha pointi 34.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Tshishimbi alisema Lipuli ni timu nzuri, ikiwa na wachezaji imara na mara nyingi wanapokutana nao, lazima mchezo uwe na ushindani.

“Tumeweza kupata ushindi katika mchezo huu lakini kocha wetu alituambia tupambane kipindi cha kwanza ili tuweze kupata mabao kwani wapinzani wetu wanaweza wakabadilika zaidi kipindi cha pili,” alisema.

Alisema licha ya kushinda, kuna baadhi ya makosa walikuwa wakifanya na kusababisha kukosa nafasi nyingi za mabao walizopata.

Tshishimbi alisema kwa sasa wataendelea kupambana ili waweze kupata ushindi katika mechi zinazowakabili ili wajikite katika nafasi ya juu kwenye msimamo wa ligi.

Mchezaji huyo aliwataka mashabiki wao kuendelea kuwapa sapoti katika mechi zao ili wapate morali na kuendeleza ushindi kwa kila timu watakayokutana nayo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles