27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 16, 2024

Contact us: [email protected]

Tshabalala kumalizana na Simba baada ya Afcon

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

BEKI wa Simba, Mohamed Hussein, ‘Tshabalala’, amesema amethibitisha kufanya mazungumzo na waajiri wake hao, lakini anatarajia kukalizana nao baada ya michuano  ya mataifa ya Afrika (Afcon).

Tshabalala ni miongoni mwa wachezaji 39 wa kikosi cha awali cha timu ya Taifa, Taifa Stars walioko kambini katika Hoteli ya WhiteSands wakijinoa kwa Afcon, ambayo inatarajia kuanza Juni 21 na kumalizika Julai 10, nchini Misri.

Beki  huyo wa kushoto pamoja na Haruna Niyonzima, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe na makipa Aishi Manula na Said Mohammed ni miongoni mwa wachezaji wa Simba waliomaliza mikataba yao msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulipofikia tamati. .

Akizungumza na MTANZANIA jana, Tshabalala alisema tayari ameanza mazungumzo na klabu hiyo kuangalia uwezekano wa kuongeza mkataba mwingine lakini zoezi rasmi la kuanguka saini anatarajia kulifanya baada ya Afcon.

“Nimeshafanya mazungumzo na viongozi, kila kitu kitakuwa wazi baada ya Afcon kumalizika,” alisema Tshabalala ambaye  pia mchezaji wa zamani wa Kagera Sugar.

Tshabalala ni moja ya mabeki wanaotegemewa katika kikosi  cha Simba  chenye makao yake makuu Msimbazi , Dar es Salaam.

Msimu  iliopita alikuwa katika kiwango bora kilichoisaidian Simba kutete ubingwa wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na kufika robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles