TSHABALALA AZOA MAMILIONI MSIMBAZI

0
640
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi (katikati), akimkabidhi beki wa Simba, Mohammed Hussein 'Tshabalala' tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu wa klabu hiyo, baada ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na uongozi wa klabu Dar es Salaaam juzi usiku. Kulia ni Rais wa Simba, Evans Aveva.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi (katikati), akimkabidhi beki wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu wa klabu hiyo, baada ya futari ya pamoja iliyoandaliwa na uongozi wa klabu Dar es Salaaam juzi usiku. Kulia ni Rais wa Simba, Evans Aveva.

 

 

Na SAADA SALIM-DAR ES SALAAM

MWENYE nacho huongezewa. Hivi ndivyo unavyoweza kumzungumzia beki wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala`, ambaye ameibuka mchezaji bora wa msimu kwa mara ya pili na kujizolea mamilioni ya fedha.

Tshabalala hivi karibuni alitangazwa kuwa mchezaji bora wa msimu na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi Kuu na kujinyakulia Sh 1,000,000 kutoka kwa mdhamini wa ligi hiyo, Vodacom.

Pia juzi katika hafla ya Iftari iliyoandaliwa na Simba, beki huyo alitangazwa rasmi kuwa mchezaji bora kwa msimu huu katika klabu hiyo kwa kujikusanyia Sh 1,000,000 na tuzo.

Katika hafla hiyo, baadhi ya mashabiki na wanachama walijitokeza kwa kumpa fedha, akiwamo Katibu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dionis Malinzi, aliyetoa Sh 1,000,000 kwa ajili ya kumpa mchezaji huyo, huku akitoa Sh 500,000 kwa Mosses Kitandu, aliyeibuka mchezaji bora kwa timu ya vijana.

Mbali na hao, pia kuna baadhi ya wanachama nao walijitokeza kutoa fedha, huku mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji wa timu hiyo, Salim Tryagain, alitoa dola 100 na kumkabidhi mchezaji huyo.

Fedha hizo zilitoka baada ya mchezaji huyo kwenda mbele kupokea tuzo yake akiwa na magongo mkononi, kutokana na majeraha aliyoyapata katika mchezo wa Fainali ya Kombe la FA kati ya Simba na Mbao FC.

Tshabalala, akizungumza baada ya kupokea tuzo na fedha hizo, alisema hajisikii vibaya kuumia akiwa anapigania timu yake, kwa kuwa wametwaa ubingwa wa FA.

“Napata maumivu ya kawaida, ila sijisikii vibaya wakati tumeshapata kombe na mwakani tuna uhakika wa kushiriki michuano ya kimataifa, hali hiyo inanipa faraja kwamba nimeumia kwa sababu maalumu,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here