22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

TRUMP: WALIMU WAPEWE BUNDUKI KULINDA WANAFUNZI

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS Donald Trump amesema kuwapatia walimu silaha kutawezesha kuzuia mashambulio ya risasi shuleni kama lile lililoua watu 17 wiki iliyopita mjini Florida.

“Mwalimu mwenye bunduki anaweza kukabiliana na washambuliaji mara moja,’, alisema Trump akitoa pendekezo hilo huku walionusurika na shambulio hilo la Februari 14 wakimtaka kuhakikisha matukio kama hayo hayatokei tena.

Rais huyo kutoka Chama cha Republican, pia aliunga mkono wito wa kuwakagua wanakotoka wanunuzi wa bunduki.

“’Tutakuwa thabiti iwapo kutakuwa na ukaguzi mbali na hali ya kiakili ya mtu anayetaka kumiliki bunduki,” alisema Trump akizungumza na wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Marjory Stoneman Douglas Ikulu mjini hapa juzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles