31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 21, 2021

TRUMP: TUTAIDHIBITI KOREA KASKAZINI

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS, Donald Trump, amesema Marekani itajiandaa kuchukua hatua dhidi ya vitisho vya nyuklia vinavyofanywa na Korea Kaskazini peke yake.

Katika mahojiano na Gazeti la Financial Times, Trump amenukuliwa akisema iwapo China haitafanya chochote dhidi ya Korea Kaskazini, Marekani itachukua hatua za upande mmoja.

Majaribio ya makombora ya hivi karibuni yaliyoendeshwa na Korea Kaskazini, yatawakutanisha kwa mara ya kwanza Trump na Rais mwenzake wa China Xi Jinping wiki hii.

Wakati wa mkutano wao mjini Florida Alhamisi na Ijumaa hii, viongozi hao wanatarajiwa kuzungumzia masuala kadhaa, mbali ya Korea Kaskazini ni kuhusu biashara na mzozo wa eneo la Bahari ya Kusini mashariki mwa China.

Katika ziara yake ya kwanza katika bara la Asia, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex Tillerson amesema diplomasia ya miaka 20 ya nchi za magharibi iliyolenga kuidhibiti Korea Kaskazini imeshindwa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,682FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles