28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 23, 2021

TRUMP: NINGEPENDA KUKUTANA NA KIM JONG-UN

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema angependa kukutana na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, iwapo kungekuwa na mazingira mahususi.

“Kungekuwa na hali mahususi kwangu kukutana naye, ningefanya hivyo bila shaka. Ingekuwa heshima kuu kwangu kufanya hivyo,” Trump aliliambia Shirika la Habari la Bloomberg jana.

Juzi Jumapili, Trump alimwelezea Kim kama ‘kijana mwerevu’.

Tamko la Trump limetokea huku wasiwasi ukiendelea kuongezeka kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Ikulu ya Marekani ilitoa taarifa baadaye kufafanua matamshi ya Trump, ikisema Korea Kaskazini ingehitaji kutimiza masharti mengi kabla ya mkutano kati ya viongozi hao wawili.

Msemaji wa Ikulu, Sean Spicer, alisema Washington inataka kuona tabia ya uchokozi ya Korea Kaskazini ikikoma mara moja.

“Ni wazi kwa sasa hakuna mazingira mahususi ya kufanikisha mkutano kama huo,” aliongeza.

Kwenye mahojiano na CBS mwishoni mwa wiki, Trump alipoulizwa kuhusu Kim, alisema: “Watu wanajiuliza je, ana akili timamu? Hilo mimi sijui. Lakini kumbuka alikuwa kijana mdogo wa miaka 26 au 27 pale baba yake alipofariki dunia.

“Bila shaka amekuwa akikabiliana na watu wakali na wagumu, hasa majenerali wa taifa hilo na wengine. Na akiwa na umri mdogo, aliweza kudhibiti madaraka.

“Nina uhakika watu wengi walijaribu kumpokonya madaraka, iwe mjomba wake au watu wengine. Na alifanikiwa kuchukua na kuyadhibiti madaraka hayo. Kwa hiyo, bila shaka, ni kijana mwerevu.”

Wakati huo huo, maofisa wa Korea Kusini wamesema ndege mbili za Marekani za kuangusha mabomu zimeruka juu ya anga la rasi ya Korea.

Kuruka kwa ndege hizo kumetokea wakati ambao Trump ametoa taarifa za kukanganya kuhusu msimamo wake kuhusu Pyongyang.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,900FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles