TRUMP: NINA MATUMAINI KIDOGO MKUTANO WANGU NA PUTIN WASHINGTON, MAREKANI

RAIS wa Marekani, Donald Trump amesema ana matumaini madogo kuhusu mkutano wake na Rais wa Urusi, Vladmir Putin utakaofanyika Finland leo.

Lakini amekiambia kituo cha habari cha CBS kuwa hakuna kilichoharibika na labda kutaibuka jambo zuri kutokana na mkutano huo.

Amesema pia ataibua suala la maofisa 12 wa usalama wa Urusi walioshutumiwa kufanya udukuzi uliomnufaisha wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka 2016.

Wito umekuwa ukitolewa nchini hapa ukimtaka Trump kuahirisha mkutano wake na Putin kutokana na shutuma zilizotolewa siku ya Ijumaa na Naibu Mwanasheria wa Serikali ya Marekani, Rod Rosenstein.

Lakini Trump amesema anaamini katika mikutano na kwamba mikutano yake na viongozi wa Korea Kaskazini na China ilikuwa kitu kizuri.

“Nafikiri ni jambo zuri kukutana. Ninaamini katika mikutano, naamini mkutano na Kim ni jambo zuri, pia mkutano na Rais wa China lilikuwa jambo zuri.”

“Hivyo kuwa na mkutano na Urusi, China na Korea Kaskazini, ninaamini kwenye hayo, hakuna jambo baya litakalojitokeza kutokana na kukutana kwetu, labda ‘jambo zuri litajitokeza,” alisema Trump

“’Siwezi kusema nini kitatokea, lakini naweza kukwambia ninachokiombea, na tutaona kama kuna jambo litatokea”.

Trump alirudia kauli yake ya kukosoa utawala wa mtangulizi wake Barack Obama, ambaye alikuwa madarakani wakati vitendo vinavyodaiwa kuwa vya udukuzi vilipofanyika.

“’Hili lilikuwa wakati wa utawala wa Obama, walikuwa wanafanya chochote walichokuwa wanataka,” alisema.

Shutuma zinadai raia wa Urusi walianza mashambulizi ya mtand eleleza Mwenyekiti wa Democratic na kuingia kwenye kompyuta za chama hicho.

Viongozi wakuu wa Democrat akiwemo mwenyekiti wa chama Tom Perez wamemtaka Trump kuachana na mazungumzo hayo akidai kuwa Putin ‘si rafiki wa Marekani’.

Kwa upande wa Republican, Seneta John Mccain amesema mkutano usiendelee isipokuwa tu kama Rais amejiandaa kumwajibisha Putin.

Siku ya Ijumaa, watu 32 wengi wakiwa raia wa Urusi walishtakiwa bila wao kuwepo mahakamani kadhalika kampuni tatu na washauri wanne wa zamani wa Trump.

aoni Machi 2016 kwenye anuani za barua pepe za wafanyakazi waliokuwa katika Kampeni za Urais za Hillary Clinton.

Wanashutumiwa kutumia mfumo uitwao, Keystroke kump