23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

TRUMP: MILIMA YA GOLAN INAMILIKIWA NA ISRAEL SIO SYRIA

Na Mwandishi Wetu

Rais Donald Trump wa Marekani amebadilisha sera ya miongo kadhaa ya Marekani kwa kusema kuwa ni wakati wa kuitambua Israel kama mmiliki halisi wa milima ya Golan ambayo iliiteka kutoka kwa Syria 1967.

Rais Trump alitangaza kwamba milima hiyo ni muhimu sana katika usalama wa Israel na uthabiti wa eneo la mashariki ya kati.

Israel iliunganisha milima hiyo na taifa lake hatua ambayo haikuungwa mkono na jamii ya kimataifa.

Syria ambayo imekuwa katika harakati za kuikomboa milima hiyo haijatoa tamko lolote.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ambaye ameonya kuhusu Iran kuingilia vita vya Syria alituma ujumbe wa shukran kwa bawana Trump kupitia mtandao wa twitter.

”Katika wakati ambapo Iran inataka kuitumia Syria kama eneo la kuikabili Israel, Trump aliitambua Israel kama mmiliki rasmi wa milima ya Golan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,411FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles