23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Trump: Marekani imepata heshima maambukizi ya corona

 WASHINGTON, MAREKANI 

RAIS wa Marekani, Donald Trump amesema ni ‘’ ni heshima ‘’Marekani ina idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona duniani. 

‘’Ninalitazama suala hili kama heshima fulani, kama jambo zuri kwasababu inamaanisha kuwa vipimo vyetu viko vizuri,’’ alieleza akiwa Ikulu ya Marekani. 

Marekani ina watu milioni 1.5 walioathiriwa na virusi vya corona na karibu vifo 92,000, kwa mujibu wa takwimu zinazokusanywa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins. 

Nchi inayoshika nafasi ya pili, ni Urusi ikiwa na maambukizi ya watu 300,000. 

Jumatatu Rais ,Trump alikuwa akizungumza mkutano wake wa kwanza wa baraza la mawaziri tangu kuanza mlipuko wa virusi nchini humo. 

Aliwaambia waandishi wa habari, ‘’Unajua unaposema tunaongoza kuwa na watu wengi walioambukizwa, ni kwa sababu tuna vipimo vingi kuliko mtu mwingine yeyote. 

‘Virusi vya corona vimefichua uongozi wa Trump kuwa haujui unachofanya’ 

Trump anakunywa ‘dawa ya corona’ isiyothibitishwa 

‘’Sijali. Ninachotaka nikupata chanjo tu inayofanya kazi” 

‘’Hivyo tuna watu wengi walioambukizwa,’’ aliendelea, ‘’Sitazami kama jambo baya, ninalitizama kwa heshima fulani, kama jambo jema kwa sababu ina maanisha kuwa tuna vipimo vizuri.’’ 

Aliongeza: ‘’Hivyo ninaliona kama nembo ya heshima. Kweli ni heshima. 

‘’Ni heshima kwa vipimo na kazi ambayo wataalamu wameifanya.’’ 

Kwa mujibu wa kituo cha kupambana na kudhibiti magonjwa , Marekani imepima watu milioni 12.6 mpaka siku ya Jumanne. 

Rais Trump, alikuwa akijibu swali kuhusu kama alikuwa akifikiria kuweka marufuku ya kusafiri kwenda Amerika ya Kusini hasa Brazil. Nchi hiyo ni ya tatu kwa kuwa na idadi kubwa ya waathirika. 

Kamati ya uongozi ya kitaifa ya Chama cha Democratic, imekosoa kauli ya Rais Trump, ikisema kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa na waathirika wa Covid-19 milioni 1.5 nchini Marekani kunaonesha ‘’kushindwa kabisa kwa uongozi’’. 

Wakati Marekani, ikiwa imefanya vipimo zaidi kuliko nchi nyingine yoyote, si ya kwanza duniani kwa ulinganifu wa idadi ya watu na vifo nchini humo kwa mujibu wa takwimu za chapisho la kisayansi la Our World in Data la Chuo Kikuu cha Oxford. 

Katika chati, Marekani ya 16 kwa vipimo kwa watu 1,000 ikiwa mbele ya Korea Kusini, lakini nyuma ya Iceland, New Zealand, Urusi na Canada. 

Katika kipindi cha juma lililopita, Marekani imekuwa ikifanya vipimo kwa watu 300,000 na 400,000 kwa siku, kwa mujibu wa mradi uitwao Covid Tracking, zikiwa ni jitihada za watu waliojitolea. 

Mkurugenzi wa Taasisi ya Afya ya Global Health, Ashish Jha wiki iliyopita aliuambia mkutano wa Congress kuwa: ‘’Marekani inahitaji vipimo zaidi ya 900,000 kila siku. Kwa sasa tuna theluthi tu ya vipimo.’’ 

Marekani pia imeripoti vifo vingi vinavyotokana na virusi vya corona kuliko nchi nyingine yoyote, ingawa kwa ulinganifu wa idadi ya watu na vifo Marekani ni ya sita nyuma ya Ubelgiji, Uingereza na Ufaransa kwa mujibu wa takwimu za Chuo cha Johns Hopkins 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles