24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

TRUMP KUWEKA MASHARTI KWA WAISLAMU KUINGIA MAREKANI

Rais wa Marekani, Donald Trump (wa tatu kushoto), akiwaita waandishi wa habari waliokuwa wakiondoka (hawapo pichani) wakati wa mkutano wake na viongozi wa wafanyakazi Ikulu mjini Washington juzi.

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS Donald Trump anatarajia kutia saini amri kuu ya kuweka masharti kuhusu wahamiaji na Waislamu kutoka baadhi ya nchi wanaoingia Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu ya Matekani, Trump alitarajiwa kuanza hatua ya kuimarisha usalama katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico alipozuru makao makuu ya Wizara ya Usalama wa Ndani jana.

Aidha, alitarajiwa pia kutoa tangazo la kuidhinisha sheria kali zaidi za kupata viza kwa wageni kutoka mataifa ya Mashariki ya Kati na Afrika yenye Waislamu wengi.

Miongoni mwa nchi zitakazoathiriwa na agizo la Trump ni pamoja na Syria, Yemen na Irak.

Trump aliandika kwenye mtandao wake wa Twitter kwamba leo (jana) itakuwa siku muhimu zaidi kwa usalama wa taifa la Marekani.

Mwandishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) aliyepo hapa, David Willis alisema hatua hiyo huenda ikayaudhi mashirika ya kibinadamu na yale ya kutoa misaada kwa kuzingatia mzozo unaoendelea sasa kuhusu hali ya wakimbizi wa Syria.

Wakati wa kampeni yake ya urais, Donald Trump aliahidi kufanyia mageuzi suala la uhamiaji Marekani.

Aligusia ujenzi wa ukuta kati ya Mexico na Marekani kuzuia wahamiaji haramu na kuwapiga marufuku Waislamu kuingia katika taifa hilo kama sehemu ya vita dhidi ya ugaidi.

Baadaye alibadili msimamo kidogo na kufafanua kwamba watakachofanyiwa Waislamu ni kufanyiwa ukaguzi mkali kabla ya kuruhusiwa kuingia Marekani.

Ubaguzi wa kidini unapigwa marufuku kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, lakini inadhaniwa utawala wa Trump utaidhinisha marufuku hiyo kwa misingi wa hatua za dharura za kukabiliana na tishio lililopo la ugaidi.

Aidha alisema kutakuwa na mikakati ambayo pia italazimu miji mitakatifu nchini Marekani kushirikiana na mamlaka katika kuwarejesha makwao wahamiaji haramu.

Miji mitakatifu ni maeneo ambayo hayakamati ama kuwazuilia wahamiaji wanaoishi katika taifa hilo kinyume na sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles