27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, November 7, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP KUWEKA KODI MPYA TEKLONOJIA KUTOKA CHINA

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS Donald Trump anajiandaa kuchukua hatua dhidi ya sekta za teknolojia na mawasiliano ya simu nchini China.

Hatua hiyo inakuja baada ya maofisa wake waandamizi wa masuala ya biashara kuwasilisha kwake viwango vikubwa vya kodi dhidi ya taifa hilo.

Kupitia mpango huo, kiasi cha dola bilioni 30 zinatarajiwa kukusanywa kutokana na ushuru utakaotozwa kwa bidhaa zinazohusu sekta ya teknolojia na mawasiliano zinazoingizwa nchini Marekani kutoka China.

Hatua hiyo inakuja wakati ambao Marekani inazituhumu kampuni za teknolojia za China kuzitaka zile za kwao kutoa siri zao za kiteknolojia kabla ya kuruhusiwa kuendesha shughuli nchini humo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayohusika na masuala ya kodi, Kevin Brady, amewaambia waandishi wa habari Rais Trump amedhamiria kupambana dhidi ya tuhuma hizo za wizi wa teknolojia.

Hata hivyo, hatua hiyo inatarajia kuibua mzozo wa kibiashara baina ya mataifa hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles