26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

TRUMP KUMSAIDIA EL-SISI

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema anapanga kuimarisha uhusiano baina yake na Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi.

Viongozi hao walijadili mapambano dhidi ya itikadi kali za Kiislamu pamoja na uchumi unaoyumba nchini Misri wakati wa mkutano wao Ikulu ya Marekani, White House mjini hapa jana.

Ni ziara ya kwanza kufanywa na kiongozi wa Misri nchini hapa kwa karibu muongo mmoja.

Rais wa zamani Barack Obama hakuwahi kumwalika el-Sisi katika Ikulu ya Marekani huku kukiwa na wasi wasi juu ya rekodi ya haki za binadamu ya serikali yake.

Lakini Trump amesema ana nia ya kujenga upya uhusiano huo.

Wakati huo huo mfalme wa Jordan Abdullah II  alikutana na Rais Trump baadaye jana kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwamo ombi la mataifa ya Kiarabu kuitambua Israel ili liundwe taifa la Wapalestina.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,388FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles