27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Trump kuanza kuwafukuza watu wasio na vibali vya kuishi Marekani

WASHINGTON- Marekani

UTAWALA wa Rais Donald Trump unapanga kuanza utekelezaji wa operesheni ya nchi nzima inayolenga familia za wahamiaji, licha ya kupingwa vikali na chama pinzani cha Democrats.

Operesheni hiyo inasemekana inaweza kuanza kutekelezwa siku mbili hizi, baada ya kuahirishwa na Trump mwishoni mwa mwezi uliopita.

Inaelezwa kuwa operesheni hiyo inalenga kuwafuatilia watu walio na amri za mwisho za kurejea katika nchi zao, zikiwemo familia za wahamiaji ambazo kesi zao zilikuwa zikifutiliwa haraka na majaji katika jumla ya miji 10 ya  Chigaco, Los Angeles, New York na Miami.

Hatua hizo zimeibua hasira na wasiwasi miongoni mwa wanaharakati wa haki za wahamiaji na wabunge. Operesheni hiyo ni sawa na ile iliyowahi kufanywa mwaka 2003 na kisha kuwakamata watu wengi wasio na vibali.

Trump alitangaza kwenye Twitter mwezi uliopita kwamba operesheni hiyo itakuwa ni mwanzo wa kuwafukuza mamilioni ya watu wanaoishi Marekani kinyume cha sheria.

Wiki mbili zilizopita

Marekani iliilazimisha, Mexico  kukubali kuchukua  hatua isiyo ya kawaida  itakayosaidia kupunguza wimbi kubwa la wahamiaji kwenda Marekani  ili kuepuka vitisho vilivyotolewa na Rais Trump la ongezeko la ushuru wa bidhaa.

Marekani na Mexico zilingia katika mazungumzo juu ya suala la kudhibiti wahamiaji haramu.

Kupitia akaunti yake ya Twitter, Rais Trump aliandika maandiko kadhaa, akibainisha kuwa  anasitisha mpango wa kuzuia ongezeko la  ushuru kwa muda usiojulikana baada ya kukubaliana na Mexico juu ya suala hilo la wahamiaji haramu.

Kama njia ya kuishinikiza Mexico kuzuia wimbi kubwa la wahamiaji wake haramu nchini Marekani, Trump alitishia kongeza ushuru wa asilimia tano kila mwezi katika bidhaa za nchi hiyo.

Katika azimio lao la pamoja,  nchi hizo mbili zilisema Mexico itachukua hatua kali kudhibiti  wahamiaji haramu na biashara ya binadamu.

Marekani pia ilikubali kutanua programu yake ya kuwarudisha wakimbizi Mexico wakati wakisubiri malalamiko yao kupitiwa.

Nchi zote mbili zimekubaliana kuimarisha ushirikiano  ikiwa ni pamoja na kuratibu hatua fulani fulani pamoja na kushirikiana taarifa.

Pia waliazimia majadiliano kuendelea,  na kwamba makubaliano ya mwisho yatatangazwa ndani ya siku 90 tangu kikao hicho kilipomalizika wiki mbili zilizopita.

Wastani wa watu milioni moja wanatajwa kupita kila mwaka katika mpaka kati ya Mexico na Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,404FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles