Trump ‘huenda hakulipa ushuru kwa miaka kadhaa’

0
473

donald-trump-bankruptcy-lies-rNEW YORK, MAREKANI

MGOMBEA Urais wa Marekani kupitia Chama cha Republican, Donald Trump, huenda hakulipa ushuru kwa miaka kadhaa kutokana na hasara kubwa ya kibiashara aliyoipata, Gazeti la New York Times linaripoti.

Linasema limepata nyaraka zinazoonyesha Trump alikuwa ametangaza kupata hasara ya zaidi ya dola milioni 900 mwaka 1995, kitu kilichomwezesha bilionea huyo wa New York kutolipa ushuru kwa zaidi ya miaka 18 kisheria.

Timu ya Kampeni ya Trump ambayo imekataa kutoa rekodi zake za nyuma kuhusu kodi, haikukubali wala kukana hasara ambazo Trump amezipata.

Katika taarifa hiyo, ilisema Trump ni mfanyabiashara hodari ambaye alijua sheria kuhusu ulipaji ushuru zaidi ya mtu yeyote yule ambaye amewahi kugombea urais.

Mpinzani wake katika kinyang’anyiro cha urais kutoka Democratic, Hillary Clinton, ameanika wazi rekodi zake za kodi.

Wakati wa mdahalo wao wa kwanza wa urais Jumatatu wiki iliyopita, alimlazimisha ajitetee kuhusu kutotoa kwake marejesho yake ya kodi, akimshambulia kwamba usiri huo huenda kuna kitu anaficha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here