27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Trump azidi kuweka ngumu makubaliano kibiashara na China

TOKYO, JAPAN

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema nchi yake haiko tayari kufikia makubaliano ya kibiashara na China, lakini anaacha wazi uwezekano wa mataifa hayo mawili siku moja kufikia makubaliano.

Akizungumza jana mjini hapa, Rais Trump alisema China iko tayari kufikia makubaliano, lakini Marekani haiko tayari.

Mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani, yamekuwa katika mzozo wa kibiashara kwa muda mrefu ambapo kila upande umekuwa ukiiwekea vikwazo biashara ya upande mwingine.

Rais Trump anatarajiwa kukutana na Rais wa China, Xi Jinping mwezi ujao katika mkutano wa mataifa yenye nguvu kiuchumi – G20.

Aidha, Rais Trump pia jana alikutana na Mfalme Naruhito wa Japan katika kasri la kifalme.

Mfalme huyo pamoja na mkewe, Masako wamemkaribisha Trump akiwa kiongozi wa kwanza wa kigeni tangu Naruhito alipotawazwa hivi karibuni.

Mbali na mfalme huyo, Rais Trump pia alikutana na Waziri Mkuu, Shinzo Abe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles