23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Trump awafukuza maofisa waliotoa ushahidi dhidi yake

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS Donald Trump wa Marekani amewafukuza kazi maofisa wawili waandamizi waliotoa ushahidi dhidi yake katika kesi ya kutokuwa na imani naye iliyokuwa inamkabili.

Balozi wa Marekani kwa Muungano wa Ulaya, Gordon Sondland, amesema “Nimeambiwa kwamba rais anataka nirudi nyumbani mara moja”.

Awali, Luteni kanali Alexander Vindman, mtaalamu mkuu katika masuala ya Ukraine, alisindikizwa kutoka nje ya Ikulu ya Marekani.

Inasemekana Trump amesema anataka kufanya mabadiliko baada ya Bunge la Seneti kumwondolea mashtaka yaliyokuwa yanamkabili Jumatano.

Katika kura ya kihistoria iliyopigwa, Bunge la Seneti limeamua kutomuondoa rais huyo wa 45 wa Marekani madarakani kwa madai yaliyokuwa yameibuliwa dhidi yake kutokana na mawasiliano yake na Ukraine.

Kaka yake, Luteni kanali Vindman ambaye pia ni pacha mwenzake, Yevgeny Vindman, wakili mwandamizi katika baraza la Usalama la taifa pia alirejeshwa katika idara ya jeshi Ijumaa.

SONDLAND

Katika taarifa iliyotolewa na wakili wake, Sondland amesema: “Nimearifiwa hii leo kwamba rais anataka nirudi nyumbani mara moja baada ya kunivua wadhifa wa balozi wa Marekani kwa Muungano wa Ulaya.

“Nashukuru kwa fursa ambayo Rais Trump alinipa ya kuhudumia taifa, pia namshukuru Waziri wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo kwa kuniunga mkono, na tena shukrani zangu ziwaendee wafanyakazi wote wa ubalozi wa Muungano wa Ulaya kwa utalaamu wao na kujitolea kwao.

VINDMAN ALIVYOONDOLEWA Mshauri wa Luteni kanali Vindman, David Pressman, ameiambia BBC kwamba mteja wake ametolewa nje ya Ikulu ambako amekuwa akifanya kazi yake kwa uadilifu na kwa nchi yake na kwa rais wake”.

“Hakuna raia yeyote wa Marekani anayejiuliza kwanini raia huyu amefutwa kazi, kwanini nchi hii sasa ina mtu mmoja tu mwenye nguvu anayeongoza Ikulu ya Marekani,” taarifa hiyo imesema.

“Luteni Vindman alifutwa kazi baada ya kusema ukweli Heshima yake, kujitolea kwake kufanya kilicho sawa, kulitia hofu wenye nguvu.”

Taarifa hiyo imeongeza:

 ” Ukweli umemgharimu kazi yake, taaluma yake, na faragha yake.”

Alexander Vindman alikuwa mtaalamu wa masuala ya Ukraine ndani ya Baraza la Usalama wa Taifa Marekani

Luteni kanali Vindman alifika kazini Ijumaa katika Ikulu kama kawaida.

Wakati anaondoka Ikulu Ijumaa kuelekea North Carolina,  Trump aliwaambia wanahabari: “Sina furaha na yeye Mnadhani kwamba nitakuwa namfurahia? hapana.”

Kulingana na vyanzo vya Ikulu ya Marekani, Luteni kanali Vindman amekuwa akitarajia kuhamishwa. 

Kwa wiki kadhaa sasa amekuwa akiwaarifu wafanyakazi wenzake kwamba yuko tayari kurejea katika idara ya ulinzi, ambako bado anatekeleza majukumu yake ya kijeshi.

Mapema Ijumaa, Waziri wa Ulinzi Mark Esper aliwaambia wanahabari kwamba idara yake inawakaribisha wafanyakazi wake wote waliokuwa wamepewa majukumu mengine.

“Kama nilivyosema, tunalinda maafisa wetu kutokana na matukio ya ulipizaji kisasi ama kitu chochote kile cha aina hiyo,” Esper aliongeza.

Walipokuwa wanatoa ushahidi wao bungeni Novemba mwaka jana,  Sondland alikuwa muwazi kabisa katika ushahidi wake kwamba ujio wa rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine katika Ikulu ya Marekani ulifikiwa kwa masharti tu kwamba nchi hiyo itaanzisha uchunguzi ambao utamsaidia Rais Trump kisiasa.

Wakati huo huo, Sondland alikuwa akifanyakazi na wakili binafsi wa Trump, Rudy Giuliani, kuhusiana na sera ya Ukraine kwa mwongozo wa rais.

Luteni kanali Vindman pia naye alitoa ushahidi Novemba mwaka jana. 

Alisema alikuwa na wasiwasi baada ya kusikia mazungumzo ya simu ya Trump ambayo hayakuwa yakawaida Julai 25, na Rais wa Ukraine.

Simu hiyo ndio chanzo cha kura ya kutokuwa na imani na Trump.

Baada ya kuulizwa ni vipi alikabiliana na hofu ya kutoa ushahidi wake, Luteni kanali Vindman alisema: “Ni kwasababu hii ni Marekani… na hapa ukweli ni muhimu sana.”

Siku moja kabla ya kuwatimua, Trump alisema kwamba mapacha hao Vindman wameshirikiana na maadui zake wa kisiasa katika Ikulu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles