29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Trump atofautiana na majasusi wa Marekani kuhusu chanzo cha virusi vya corona

 WASHINGTON, MAREKANI

RAIS wa Marekani, Donald Trump ametofautiana na Idara ya intelijensia ya nchi hiyo kuhusu chanzo cha virusi vya corona akidai kuwa ana ushahidi virusi hivyo vilitengenezwa katika maabara ya China.

Awali ofisi ya mkurugenzi wa shirika la ujasusi ilisema bado inachunguza chanzo cha virusi hivyo.

Lakini ofisi hiyo ilisema kuwa haijabaini ikiwa Covid-19 “ilitengenezwa na binadamu au kupitia mfumo wa maabara”.

China imepinga madai kuwa maabara yake ni chimbuko la virusi hivyo na kuikosoa Marekani kuhusu kauli yake juu ya ugonjwa wa Covid-19.

Tangu mlipuko wa ugonjwa huo ulipotokea katika mji wa Wuhan nchini China mwishoni mwa mwaka uliopita, watu milioni 3.2 duniani wamethibitishwa kuwambukizwa virusi vya corona na zaidi ya watu 230,000 kufariki.

Akihutubia wanahabari katika Ikulu ya White House Alhamisi, Trump aliulizwa : “Je una uhakika gani kwamba Taasisi ya Virology ya Wahun ni chimbuko la virusi vya corona?”

“Ndio, nina hakika. Ndio, nina hakika,” alisema Rais Trump, bila kutoa ufafanuzi zaidi.

“Nadhani Shirika la Afya Duniani linastahili kujitathmini zaidi kwasababu limekuwa kama shirika la uhusiano mwema la China.”

Alipolizwa kufafanua maelezo yake, alisema: “Siwezi kuwaambia hilo. Siruhusiwi kuwaambia kuhusu hilo.”

Aliwaambia waandishi wa habari pia: “Hata kama wachina walifanya hivyo bila kukusudia au walikosea na kutengeneza nyingine, au walianza kutengeneza kwa bahati mbaya au kuna mtu aliteyengeneza kwa kudhamiria?

“Sielewi ni kwa nini watu hawaruhusiwi kwenda kupumzika China lakini wanaruhusiwa katika maeneo mengine ya dunia.Jambo hilo ni baya na swali gumu kwa wao kujibu.”

Gazeti la New York Times siku ya Alhamisi liliripoti kuwa maofisa wa ngazi ya juu wa Ikulu ya White house waliitaka jumuiya ya intelijensia ya Marekani kuchunguza kama virusi vimetokea katika maabara ya utafiti ya Wuhan.

Wakala wa Kiintelijensia wametakiwa kudhibitisha kama China na Shirika la Afya Duniani linaficha taarifa za awali za virusi vya corona, ofisa ambaye hakuta jina lake kutajwa aliwaambia NBC News siku ya Jumatano.

Kiongozi wa intelijensia alisemaje?

Ofisi ya mkurugenzi wa taifa wa intelijensia anasema Alhamisi kuwa wamechunguza kwa kina na kuungana na wanasayansi wengine kusema kuwa asili ya ugonjwa wa Covid-19 chanzo chake ni cha asilia.

“Jumuiya ya intelijensia itaendelea kuchunguza taarifa za chanzo cha ugonjwa huu kama maambukizi yalianzia kwa wanyama au ni matokeo ya ajali ya kisayansi katika maabara ya Wuhan.”

Lilikuwa jibu la wazi kutoka intelejensia ya Marekani kuelezea madai ya kutoka katika nchi zote mbili Marekani na China – kwamba virusi hivyo ni silaha ‘bioweapon’

CHANZO CHA MVUTANO

Hivi karibuni Trump amekuwa akipambana na China kwa vita ya maneno kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa corona, ingawa utawala wa Marekani umeelezea kuwa wamepatana na China.

Siku ya Jumatano, alisema kuwa China wanataka ashindwe kuchaguliwa tena nafasi ya urais mwezi Novemba. Trump aliwahi kuwashutumu maofisa wa China walikuwa wanaficha taarifa na wangeweza kuzuia maambukizi kuenea zaidi.

Alilikosoa shirika la afya duniani WHO na kuondoa ufadhili wa taifa lake katika shirika hilo.

Wizara ya mambo ya nje nchini China ,ameushutumu utawala wa Trump kwa kujaribu kuwalaumu kwa matatizo yao wenyewe ya kushindwa kukabiliana na janga hili.

Kwa mujibu wa Washing Post, utawala wa Trump unajaribu kutafuta namna ya kuiangusha China kiuchumi.

Mjadala huo uliripoti kujumuisha madai kuwa serikali ya Marekani itaishitaki China kwa kusitisha makubaliano ya mkopo.

Propaganda za Marekani na China

Hii ni taarifa ya kwanza ambayo inajieleza vizuri kuhusu suala hilo kutoka kwa vyombo vya kijasusi nchini Marekani.

Imekuwa ikikataa nadharia zote kuhusu ukweli wa chanzo cha mlipuko huu kuwa wachina walitengeneza virusi vya corona kama silaha za bio.

Lakini kuna uwezekano kuwa kwa bahati mbaya kirusi hicho kikaingia kwenye maabara ya utafiti wa magonjwa yanayoambukiza huko Wuhan.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alizungumzia suala hilo , na kutaka China kukubali wataalamu kutoka nje ya China kuchunguza eneo hilo na swali la usalama wa maabara wa sehemu nyingine za nchi.

Serikali ya China ilisema kuwa madai kama hayo ambayo hayana ushaidi wowote na hayajengi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,882FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles