23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 12, 2024

Contact us: [email protected]

Trump atishia kuiangamiza Uturuki kiuchumi

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS wa Marekani Donald Trump ametishia kuiangamiza Uturuki kiuchumi iwapo taifa hilo litashambulia vikosi vya Wakurdi waliopo Syria baada ya askari wa Marekani kuondoka nchini humo.

Katika ujumbe wake alioutuma kwenye mtandao wa Twitter, Trump alisema hatarajii Wakurdi kwa upande wao pia kuichokoza Uturuki.

Vikosi vya Marekani vimepambana kwa ushirikiano na wanamgambo hao kaskazini mwa Syria dhidi ya kundi lijiitalo Dola la Kiislamu (IS).

Uturuki hata hivyo, inawachukulia wapiganaji hao wa wa YPG kama magaidi.

Na Rais Recep Tayyip Erdogan alizungumza kwa hasira juu ya Marekani kuliunga mkono kundi hilo, na kuapa kuliangamiza.

Kauli ya Trump juzi inafuata shutuma zaidi dhidi ya uamuzi wake wa ghafla kuondosha vikosi vya Marekani kutoka Syria.

Afisa Mkuu wa familia ya kifalme Saudia, Prince Turki al-Faisal, aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa uamuzi huo utakuwa na athari mbaya kwani huenda Iran, Rais wa Syria Bashar al Assad na Urusi zikafaidika nao.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo kwa sasa yuko katika mji mkuu wa Saudia, Riyadh katika ziara yake Mashariki ya Kati kuwahakikishia washirika wa Marekani eneo.

Rais ametetea uamuzi wake kuondoa vikosi, akieleza kuwa wapiganaji wowote waliosalia wa IS wanaweza kushambuliwa kutoka eneo ambalo halikutajwa, lililopo katika kambi za karibu.

Lakini pia hakueleza namna uchumi wa Uturuki utakavyoathirika iwapo taifa hilo litawashambulia wapiganaji wa YPG.

Msemaji wa Rais Erdogan, Ibrahim Kalin amejibu katika ujumbe wa Twitter akisema Uturuki ilitarajia Marekani ‘kuheshimu ushirikiano wetu wa kimipango’.

“Magaidi hawawezi kuwa washirika na wandani wako,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles