24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP ATANGAZA KUSUSIA HAFLA YA WANAHABARI IKULU

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS Donald Trump ametangaza kutohudhuria hafla ya kila mwaka inayoandaliwa na Chama cha Waandishi wa habari wa Ikulu ya Marekani, White House.

Hafla hiyo kwa kawaida huwavutia wageni mashuhuri, wanasiasa na waandishi wa habari.

Tangazo lake hilo limekuja wiki moja tu baada ya kuimarisha mashambulizi yake dhidi ya mashirika ya habari.

Kwa kawaida hafla hiyo ya kila mwaka ya White House hutoa nafasi kwa wanahabari na Rais kusahau tofauti zao kwa muda.

Marais 15 wamewahi kuhudhuria hafla hii ya jioni ambayo huwavutia watu wengi mashuhuri na imeendelea kwa zaidi ya miaka 100.

Hata hivyo, uhusiano kati ya waandishi na Rais Trump umezorota kwa majuma machache yaliyopita.

Rais amewasema baadhi ya wanahabari na taasisi wanazofanyia kazi kama ‘habari bandia’ na kuwataja kuwa maadui wa Marekani.

Aidha, Ijumaa iliyopita Ikulu iliwazuia kuingia ukumbini wanahabari katika mkutano wa waandishi wa Rais.

Miongoni mwao ni waandishi kutoka vyombo vya habari vya CNN, New York Times na BBC.

Hata hivyo, waandaaji wa hafla hiyo wamesema kuwa itaendelea kama ilivyopangwa Aprili 29 mwaka huu na uhuru wa vyombo vya habari utapewa kipaumbele kulingana na Katiba ya nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles