TRUMP ASITISHA CHAKULA CHA EID IKULU

0
599

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS wa Marekani Donald Trump, amevunja utamaduni wa karibu miaka 20 kwa kutoandaa chakula cha jioni kuadhimisha kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Hafla hiyo inayoandaliwa katika Ikulu ya White House imekuwa ikifanyika kila mwaka tangu kipindi cha Rais Bill Clinton.

Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson anaripotiwa kukataa ombi la kutaka hafla hiyo kuandaliwa.

Mei mwaka huu, Shirika la Habari la Reuters lilisema Tillerson alikataa pendekzeo kutoka kwa idara inayohusika na masuala ya dini ya wizara hiyo kuandaa sherehe hiyo.

Awali Trump alilaumiwa kutumia maneno makali dhidi ya waislamu ikiwemo kampeni ya kutaka uchunguzi kufanyiwa misikitini nchini Marekani.

Alisema katika taarifa: “Kwa niaba ya watu wa Marekani na Melania ninatuma heri njema kwa Waislamu wakati wanaposherehekea Eid al-Fitr.

Chakula cha kwanza cha Eid Ikulu mjini hapa kiliandaliwa na Rais Thomas Jefferson mwaka 1805 kwa ujumbe kutoka Tunisia.

Sherehe hizo zilifufuliwa tena na Hillary Clinton mwaka 1996 wakati akiwa mama wa kwanza wa taifa.

Hafla hiyo ilianza kufanywa kila mwaka tangu mwaka 1999 na kuhudhuriwa na viongozi mashuhuri wa Kiislamu nchini Marekani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here