Trump ashindwa kulipa wafanyakazi, Casino yafungwa

0
665

tajmahal

Atlantic, Marekani.

Miaka 26 iliyopita Donald Trump alifungua kiota cha maraha na kukiita ajabu la nane la dunia, lakini rafiki yake bilionea Carl Icahn amefunga Casino hiyo iliyokuwa na takriban wafanyakazi 3,000.

Casino hiyo iliyojengwa kwa mfano wa kasri maarufu la Taj Mahal la India, imefungwa leo baada ya kushindwa kufikia makubaliano na umoja wa wafanyakazi kwa kurudisha makato ya huduma ya afya na mafao kwa wafanyakazi hao.

“Tumeungana kugoma dhidi ya bilionea anayetuibia” aliseme Marc Scittina, aliyefanya kazi mahali hapo kama mhudumu wa chakula toka mwaka 1990. “”

Mvutano wa swala hilo umedumu kwa miaka miwili sasa, na kufikia Julai  Mosi mwaka huu, Umoja huo wa wafanyakazi uligoma. Hivyo, Icahn ameamua kuifunga kwa madai kuwa hawakuwa wakitengeneza faida.

“Nashangaa kwanini tumeshidwa kukubaliana wakati nina hakika kulikuwa na nafasi ya kufikia muafaka,” alisema Trump

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here