24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Trump asema corona ni shambulio baya kwa Marekani kuliko la Osama

 WASHINGTON, MAREKANI

KWA mara nyingine Rais wa Marekani, Donald Trump ameishambulia China kwa jinsi ilivyoshughulikia mlipuko wa virusi vya corona huku akisema janga hilo limekuwa na madhara makubwa kwa Marekani kuliko shambulio la kigaidi la Septemba 11, 2001.

Rais Trump aliwaambia waandishi habari mjini Washington kuwa ugonjwa wa COVID-19 umeiathrii Marekani kwa kiwango kikubwa kuliko mashambulizi ya mabomu dhidi ya kambi ya kijeshi ya Pearl Harbor ya mwaka 1941 au tukio la kigaidi la Septemba 11 lililotekelezwa na kikundi cha al-Qaeda chini ya Osama bin Laden.

Mashambulizi ya Japan kwenye kambi ya Pearl Harbor iliyokuwepo Hawaii yaliilazimisha Marekani kuingia katika vita kuu ya pili ya dunia huku mkasa wa Septemba 11 uliwaosababisha vifo vya Wamarekani zaidi ya 3,000 uliifanya nchi hiyo kuanzisha operesheni dhidi ya ugaidi nchini Iraq, Afghanistan na kwingineno.

Juzi Trump aliilaumu China akisema virusi vya corona visingesababisha athari kubwa iwapo nchi hiyo ingefanikiwa kuvidhibiti kikamilifu vilipozuka mwishoni mwa mwaka uliopita.

“Tumepatwa na shambulio kubwa zaidi kuwahi kutokea nchini kwetu, shambulio hili ni baya zaidi ya la Bandari ya Pearl. Hili baya zaidi ya la Kituo cha Biashara cha Dunia (9/11). Hatujawahi kupatwa na shambuli kama hili. 

“Na halikutakiwa kutokea, lingeweza kuzuilika kwenye chanzo chake, lingeweza kuzuiliwa na Uchina, lingeweza kuzuiliwa kwenye chanzo chake, lakini hilo halikufanyika,”alisema Trump.

Alipoulizwa iwapo analiona janga hilo kama shambulio la kivita kutoka Uchina, Trump alijibu kuwa kwa sasa adui wa Marekani ni mlipuko wa virusi na si Uchina. 

“Ninamchukulia huyu adui asiyeonekana kama vita, sipendi kabisa jinsi gani alifika hapa, kwa kuwa kulikuwa na uwezekano wa kuzuia,” alisema Trump. 

Maelezo ya Trump ni mfululizo wa lawama za Marekani kwa China kuhusu virusi vya corona na katika siku za karibuni Rais Trump na viongozi wake waandamizi wamesema wana ushahidi kuwa virusi vya corona vilizuka kutoka maabara moja mjini Wuhan nchini China. Madai hayo yamepingwa vikali na China na wanasayansi bado wanaamini virusi hivyo vialinzia kwa wanyama kabla ya kuingia kwa binadamu hususan kupitia soko la nyamapori la mjini Wuhan.

Hadi sasa zaidi ya watu 73,000 wamefariki dunia nchini Marekani kutokana na ugonjwa wa COVID-19 na mkuu wa zamani wa taasisi ya kuzuia magonjwa nchini humo amebashiri kuwa idadi ya vifo inaweza kufikia 100,000 mwishoni mwa Mei.

Hadi sasa virusi vya corona vimesababisha vifo vya watu 260,000 kote duniani huku na wengine karibu milioni 3.7 wameambukizwa maradhi ya COVID-19.

Mzozo wa Marekani na China ulizidi kukolezwa juzi baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo aliporejelea mashambulizi yake dhidi ya Uchina kwa kuwatuhumu kuficha taarifa za janga hilo.

Bado ameendelea kusema kuwa “kuna ushahidi mwingi” unaoonesha kuwa virusi hivyo vilitengenezwa kwenye maabara moja nchini Uchina japo madai hayo hayajathibitishwa.

Hata hivyo, amekiri kuwa bado kuna mashaya wapi virusi hivyo vilipochipukia

“Kauli zote mbili hizo ni sahihi, hatuna uhakika wa moja kwa moja virusi vimechipukia wapi lakini kuna ushahidi wa kutosha kuwa vilitengenezwa maabara moja nchini China,” Pompeo ameiambia BBC,

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles