25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Trump aonya kuongezeka kwa vifo

 WASHINGTON, MAREKANI

RAIS Donald Trump amewaonya Wamarekani kutarajia kipindi kigumu cha wiki mbili baada ya Ikulu kuzungumzia uwezekano wa kuongezeka kwa vifo kufuatia janga la virusi vya Corona

Ikulu ya White House inatabiri kuwa huenda idadi ya vifo vinavyotokana na virusi vya Corona ikawa kati ya watu 100,000 hadi 240,000 nchini Marekani hata iwapo miongozo iliyotolewa ya watu kukaa mbali na wenzao itazingatiwa.

Rais Trump ametilia uzito tahadhari hiyo kwa kusema ni suala la kufa na kupona. Rais huyo amewataka Wamarekani kuzingatia maagizo yaliotolewa na maafisa wa afya ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.

Tayari zaidi ya Wamarekani 3,500 wamefariki kutokana na virusi hivyo huku wengine zaidi ya 170,000 wakiambukizwa virusi hivyo.

Na nchini Saudia Arabia, waziri anayehusika na masuala ya Hijja na Umrah ametoa wito kwa waumini wa dini ya Kiislamu wanaokusudia kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu kuchelewesha kupanga safari zao, katika ishara ya uwezekano wa kufutwa kwa ibada hiyo kutokana na hofu ya kuenea kwa virusi vya Corona.

Waislamu wanaokusudia kutekeleza ibada ya Hijja washauriwa kuchelewesha kupanga safari zao

Februari mwaka huu, utawala wa kifalme nchini humo uliamua kuifunga miji mitakatifu ya Makka na Madina, hatua ambayo ililenga kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.

Miji hiyo haijawahi kufungwa hata wakati wa janga la homa ya mafua makali ya mwaka 1918 iliyojulikana kama Mafua ya Hispania, ambayo iliwaua mamilioni ya watu kote duniani.

Nchi hiyo ya kifalme imeweka vizuizi kadhaa ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona. Kwa sasa, Saudia Arabia imethibitisha zaidi ya maambukizi 1,500 ya virusi vya corona na imerekodi vifo 10 kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

Kwa ujumla eneo la Mashariki ya Kati limethibitisha zaidi ya visa 71,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona huku Iran ikirikodi visa vingi zaidi.

Na nchini Afghanistan, baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limezitolea wito pande zinazohasimiana nchini humo kuweka chini silaha na badala yake kushughulikia janga la Covid-19.

Naibu mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa, Ingrid Hayden alisema nchi hiyo imefikia hatua muhimu ambayo inastahili viongozi wake wakae katika meza moja ya mazungumzo ili kuhakikisha amani inapatikana.

Na aliyekuwa Rais wa klabu ya mpira ya Marseille Pape Diouf amefariki dunia kutokana na virusi vya Corona akiwa na umri wa miaka 68.

Diouf alikuwa amelazwa katika hospitali moja nchini Senegal baada ya kuambukizwa virusi hivyo, na anakuwa mtu wa kwanza nchini humo kufariki kutokana na ugonjwa wa Covid-19.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,526FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles