25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Trump amtishia Mkuu wa WHO kuondoa misaada yote

 WASHINGTON, Marekani

RAIS wa Marekani, Donald Trump amemtumia barua Mkuu wa Shirika la Afya duniani, (WHO), akitishia kuondoa kabisa mchango wa taifa lake kifedha kwa shirika hilo kutokana na janga la Covid-19

Barua hiyo, imelipa shirika hilo siku 30 kufanya “maboresho makubwa” au ipoteze mamilioni ya dola na hata uanachama wa Marekani kwa pamoja.

Barua iliyoelekezwa kwa mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus inakosoa awamu mbalimbali za shirika za kushughulikia janga la corona tangu Desemba, mwaka jana.

Rais Trump pia amelituhumu shirika hilo la Umoja wa Mataifa (UN) kwa ‘’kibaraka wa China’’.

Rais huyo anayekabiliwa na uchaguzi mwaka huu na yeye kukosolewa kwa namna anavyoshughulikia janga hilo, ameitupia lawama China kwa kujaribu kuficha taarifa kuhusu mlipuko wa virusi vya corona pia ameishutumu kushindwa kuiwajibisha China.

Waziri wa Afya wa Marekani pia aliitupia lawama WHO kuruhusu Covid -19 kushindwa kudhibitika kwa gharama ya maisha ya watu wengi.

 ‘’Shirika hili lilifeli kupata habari ambayo ulimwengu ulihitaji’’, alisema waziri wa Afya wa Marekani Alex Azar.

Alazar alitoa matamshi hayo katika hotuba kwenye mkutano wa UN.

Mkuu wa WHO awali alikubali kufanyika uchunguzi ambao utaweka wazi jinsi shirika hilo lilivyoangazia mlipuko huo.

Rais wa Marekani Donald Trump , ambaye anakabiliwa na uchaguzi mkuu mwaka huu ambaye amekosolewa jinsi anavyotatua ugonjwa huo nchini Marekani , amelaumu China kwa kujaribu kuziba mlipuko huo na kuilaumu WHO kwa kushindwa kuiwajibisha China.

Rais wa China Xi Jingpin , ambaye ametetea vitendo vya China wakati wa mlip[uko huo , alisema katika mkutano huo kwamba taifa lake lilikabiliana na ugonjwa huo kwa uwazi na kusisitiza kwamba uchunguzi wowote ufanyike baada ya mlipuko huo kudhibitiwa.

Aliongezea China itatoa $2bn katika kipindi cha miaka miwili ili kusaidia mataifa duniani na kutoa ombi la kugawanya chanjo itakapokuwa tayari.

Wakati huohuo rais wa Korea Kusini Moon Jae-in amesema kwamba WHO inafaa kupewa uwezo wa kisheria kuhakikisha kuwa matafa yanaripoti milipuko na kupeana data.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles