28.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Trump ammwagia sifa Kanye West

NEW YORK, MAREKANI

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amemmwagia sifa mkali wa muziki wa hip hop, Kanye West, mara baada ya msanii huyo kutangaza kuachana na masuala ya siasa.

Mapema wiki hii msanii huyo aliamua kuweka wazi kuwa alikuwa anatumika kwenye masuala ya siasa, hivyo ni wakati wa kuachana na mambo hayo na kujikita kwenye mambo yake mbalimbali.

Trump alifanya mazungumzo na waandishi wa habari wa Ikulu na kusema kwamba, Kanye West ni kijana bora na ameamua kufanya maamuzi sahihi.

Mapema mwaka huu, Kanye West, alitangaza kuwa kwenye mipango ya kuja kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2020, lakini amedai alikuwa anatumwa kuongea mambo mengine ambayo yeye mwenyewe alikuwa hayaamini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,085FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles