23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

TRUMP AMFUKUZA KAZI TILLERSON


WASHINGTON, MAREKANI   |   

RAIS wa Marekani, Donald Trump jana alitangaza kumfukuza kazi Waziri wa Mambo ya Nje, Rex Tillerson na kumteua Mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi Marekani (CIA), Mike Pompeo kushika wadhfa huo.

“Mike Pompeo, Mkurugenzi wa CIA, atakuwa waziri wetu mpya wa mambo ya nje. Atafanya kazi nzuri kweli kweli!,” Trump aliandika katika mtandao wa tweeter.

“Shukrani kwa Rex Tillerson kwa utumishi wake!” aliongeza.

Aidha, Trump amemteua Gina Haspel kuchukua wadhifa wa Pompeo na kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo.

Tillerson, afisa mkuu mtendaji wa zamani wa Kampuni ya Mafuta ya ExxonMobil, aliteuliwa kuwa mwanadiplomasia namba moja wa Marekani mwaka mmoja tu uliopita.

Ofisa mmoja mwandamizi wa Ikulu ya Marekani, alisema Rais alitaka kuhakikisha ana timu mpya tayari kwa mkutano ujao na Korea Kaskazini pamoja na majadiliano yanayoendelea ya kibiashara.

Tillerson alikuwa katika ziara rasmi barani Afrika wiki iliyopita wakati aliposhtukizwa na tangazo la Trump kuwa atafanya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un.

Mwelekeo huo unakuja huku Tillerson akiripotiwa kuugua Jumamosi iliyopita na kulazimika kupunguza ratiba ya ziara yake Afrika kwa siku moja ili kuwahi majukumu aliyoitiwa nyumbani.

Jumatatu, Tillerson alionekana akiondoka eneo la kuzungumzia Ikulu wakati alipounga mkono mamlaka za Uingereza zinazoilaumu Urusi kwa kumshambulia kwa sumu jasusi wake wa zamani nchini Uingereza.

Lakini Ikulu ya Marekani imekuwa ikigoma kuinyooshea kidole Urusi.

Ripoti zinasema Trump na Tillerson wamekuwa wakitofautiana mara kwa mara katika sera za kigeni kuanzia kuhusu Iran, Korea Kaskazini hadi Urusi na lugha ya wawili hao vikaoni imekuwa ikionyesha hilo.

Awali, Tillerson alisisitiza kuwa hana mpango wa kujiuzulu na kupuuza ripoti kuwa alimuita Trump mpuuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles