TRUMP AKANA KUHONGA VIMADA

0
735

 

WASHINGTON DC, Marekani


RAIS wa Marekani, Donald Trump,  amekana vikali tuhuma za kuhusika kwake katika kutumia fedha wakati wa mikutano ya kampeni kuwalipa wanawake wawili ambao wanasadikiwa kuwa na uhusiano naye wa  kimapenzi.

Kauli hiyo ya Trump imekuja baaada ya kesi iliyosikilizwa katika mahakama moja mjini New York mapema wiki hii , mwanasheria wa zamani wa rais Trump, Michael Cohen, kusema kuwa kiongozi huyo  alimpa maelekezo kutoa fedha kwa lengo kuu la kuwashawishi wanawake hao kukaa kimya wakati wa uchaguzi wa rais wa 2016.

Ingawa katika mahojiano na kituo cha runinga cha Fox News, Rais Trump alitoa ufafanuzi kuwa malipo hayo yalitoka katika fedha zake binafsi na hazikuwa  za kampeni kama inavyodhaniwa  na akasema kwamba  alikuja kubaini baadae juu ya  malipo hayo, ingawa hakubainisha kuwa miamala hiyo ilifanyika wakati gani.

Rais Trump amekuwa akimshutumu Cohen kwa kupika mambo dhidi yake kwa lengo la kupata huruma na kuepuka kifungo.

Hata hivyo Ikulu ya hapa White House  inamkingia kifua kiongozi huyo  ikieleza kuwa  kuvunja sheria ya fedha za kampeni kwa Michael Cohen hakumaanishi kuwa Rais Trump naye atawajibika ingwa msemaji wa Serikali  Sarah Sanders amekataa kusema ni lini rais huyo  alijua juu ya malipo ya wacheza filamu wawili wa ngono.

”Kama rais alivyosema katika matukio tofauti tofauti, hajafanya kitu chochote kibaya, hakukua na madai yoyote dhidi yake katika hili na kwa sababu tuu Michael Cohen amekiri makosa yake haimaanishi inamgusa Rais pia,” alisema msemaji huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here