22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 1, 2022

TRUMP AJICHANGANYA KAULI YAKE KUHUSU URUSI

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS Donald Trump, amesema anakubaliana na hitimisho lililotolewa na taasisi za kijasusi za nchi yake kuwa Urusi iliingilia Uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka 2016.

Kauli hiyo, inamaanisha anakana ile aliyoitoa siku moja iliyopita baada ya mkutano wake na Rais Vladmir Putin wa Urusi.

Trump amedai alieleweka vibaya siku ya Jumatatu na kwamba alikuwa akimaanisha hakuona sababu kwanini isiwe Urusi ambayo ilifanya udukuzi katika uchaguzi huo.

Kujikanganya kwa Trump kunakuja baada ya kauli yake ya awali kuzua sintofahamu na kukosolewa vikali kila upande si tu nchini Marekani, bali pia kutoka kwa washirika wake, ambao walitaka ufafanuzi zaidi na kuisafisha.

Alidai kuwa katika mkutano huo wa Helsinki, alimaanisha kusema hakuna sababu ya kufikiria kuwa Moscow haiwezi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani.

Alisema ana imani na kuunga mkono taasisi za usalama za nchi yake.

“Naanza kusema kwamba nina imani na kuunga mkono mashirika ya kijasusi ya Marekani na siku zote ni hivyo.

“Acha niweke wazi kabisa kwa kusema na nimekuwa nikisema hivyo mara kadhaa, kwamba nakubaliana na hitimisho lililotolewa na wapelelezi wetu kuwa Urusi ilifanya udukuzi katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2016,” alisema Trump.

Lakini hata hivyo baadhi ya wapinzani wake, wamesema hawana imani na utetezi huo alioutoa, huku baadhi yao wakiionya Urusi kwamba kilichotokea mwaka 2016 kisitokee tena.

Mark Warner, Seneta kutoka chama cha upinzani nchini Marekani cha Democratic, ameweka wazi kwamba hana imani na kauli za kiongozi huyo.

“Sikubaliani na kauli alizotoa rais leo (jana). Kama angetaka kutoa kauli hizo, angepaswa kuwa na uwezo wa kufanya hivyo mbele ya Vladmir Putin.

“Huyu ni Rais ambaye alionyesha udhaifu mbele ya kiongozi wa Urusi, alionyesha udhaifu mbele ya dunia nzima,” alisema Seneta Warner.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,373FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles