31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

TRUMP AIONYA EAC USITISHAJI NGUO ZA MITUMBA

WASHINGTON, MAREKANI


UAMUZI wa viongozi wakuu wa mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuharamisha uingizaji wa nguo za mitumba kuanzia mwaka ujao, umeikera Serikali ya Rais Donald Trump, ambayo imeonya inaweza kuchukua hatua.

Miongoni mwa hatua ilizopanga ni kuangalia uwezekano wa kuzuia mataifa hayo kuingiza bidhaa bila ushuru Marekani kupitia Mpango wa Ukuzaji wa Fursa za Kiuchumi Afrika (AGOA).

Kwa mujibu wa Marekani, amri ya marais wa EAC kuharamisha uingizaji wa nguo za mitumba, hautanufaisha ujio wa nguo za ziada za Marekani na za uwekezaji ukanda huo, ambazo kwa kiasi kikubwa zinauzwa nje chini ya AGOA.

Katika mkutano wa maofisa wa biashara uitwao “Marekani Nje ya AGOA – Biashara na Uwekezaji”, maofisa wa Marekani wamesema sera za uagizaji biashara kama za EAC zinazopiga marufuku nguo za mitumba, zitaifanya Washington iachane na wazo la kuwekeza eneo hilo.

Serikali ya Marekani sasa inasema itawasilisha shauri katika Ofisi ya Uwakilishi wa Biashara Marekani (USTR) kujadili tathmini mpya ya ushiriki wa mataifa ya EAC.

Iwapo EAC itaonekana haifanyi vyema kufikia masharti yaliyowekwa, Marekani huenda ikaiondoa kutoka AGOA.

Ripoti kutoka mkutano wa maofisa wa EAC na Marekani, inaonyesha jumuiya hiyo imesisitiza msimamo wa kusitisha nguo za mitumba, ikisema wakuu wa nchi wanatoa kipaumbele kwa mkakati wake wa maendeleo ya viwanda, ambavyo pia vinahusisha sekta za nguo, ngozi na magari.

Hatua za kuachana na uagizaji wa nguo za mitumba, ni sehemu ya sera ya kuendeleza viwanda katika nchi za EAC.

Na inasisitiza kuwa Marekani badala ya kulalamika, inapaswa kuona mkakati wa EAC kama fursa ya kuwekeza katika sekta ya nguo eneo hilo.

Maofisa wa EAC kwa sasa wameomba kukutana na wenzao wa Marekani kabla ya kikao kijacho cha tathmini kuhusu sifa stahili ya kujumuishwa AGOA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles