30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

TRUMP AIFUTA SHERIA YA WATOTO KUTUMIA CHOO KIMOJA

WASHINGTON, MAREKANI


RAIS wa Marekani Donald Trump amefutilia mbali sheria inayoruhusu watoto wa kike na kiume kutumia choo kimoja iliyobuniwa wakati wa utawala wa Rais Barack Obama.

Utawala wa Obama ulibuni sheria hiyo ili kuaingatia wanafunzi walioegemea jinsia zote mbili kutokana na dhana kuwa kulikuwa na ubaguzi dhidi yao.

Lakini wakosoaji wa Obama walisema sheria hiyo ilivuka mipaka kwani halikuzingatia usalama na usiri wa watoto.

Wizara ya Elimu mwaka jana ilitoa agizo lililozitaka shule kuruhusu watoto kutumia bafu au vyoo kwa kadiri ya utashi wao hasa kuendana na jinsia wanayohisi kuikumbatia zaidi.

Lakini majimbo 13 yaliwasilisha pingamizi mahakamani kuipinga sheria hiyo huku ikizua mijadala ya jinsi ya kuitekeleza.

Barua iliyotumwa kwa shule za umma nchini Marekani ilieleza mabadiliko hayo yaliyofanywa na Trump, na kuongeza kwamba agizo la Obama lilisababisha hali ya sintofahamu.

Ingawa haikuwa imefanywa kuwa sheria, Obama alizitahadharisha shule zingenyimwa ufadhili iwapo zingekiuka agizo hilo.

Mabadiliko yaliyofanywa na Trump hayatakuwa na athari kubwa kwa vile agizo la Obama lilisimamishwa kwa muda na jaji katika jimbo la Texas Agosti mwaka jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles