25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Trump aiasa Uingereza kuhusu EU

WASHINGTON, MAREKANI

RAIS Donald Trump ameliambia gazeti la Uingereza la The Sunday Telegraph katika mkesha wa ziara yake mjini London, kuwa Uingereza inapaswa kuchukua uamuzi wa kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya  (EU) bila ya makubaliano na kukataa kulipa euro bilioni 45 kama fedha ya kujitoa.

Matamshi hayo ya kiongozi huyo wa Marekani yanakuja baada ya kuliambia gazeti la The Sun la Uingereza kwamba anafikiria kwamba waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Boris Johnson kuwa atakuwa waziri mkuu bora kuchukua nafasi ya Theresa May.

May ni Waziri Mkuu wa sasa, ambaye atajiuzulu rasmi kisheria ifikapo Juni 7 baada ya kushindwa kukamilisha hatua ya kujitoa EU, yaani Brexit kupitia Bunge la nchi hiyo. 

Trump anaanza ziara ya siku tatu nchini Uingereza leo, ambapo atakutana na Malkia Elezabeth wa pili na kuwa na mazungumzo na May.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles