25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Trump agoma kuhudhuria kikao cha uchunguzi dhidi yake

WASHINGTON, MAREKANI

RIPOTI ya Baraza la Wawakilishi la Marekani kuhusu mchakato wa kumchunguza Rais Donald Trump imewasilishwa katika kikao cha faragha, lakini Ikulu ya White House imekataa mwaliko wa kushiriki.

Kamati ya masuala ya kijasusi katika Baraza la Wawakilishi ambayo inadhibitiwa na wabunge wa Chama cha Democratic, imesema ripoti hiyo iliyoandikwa kutokana na ushahidi uliotolewa kwa wiki kadhaa itazungumza yenyewe, katika kubainisha kile mwenyekiti wa kamati hiyo, Adam Schiff alichokiita “makosa na ukosefu wa maadili” vilivyofanywa na Trump katika matendo yake kuhusiana na Ukraine.

Wabunge ambao ni wanachama wa kamati hiyo walipata fursa ya kuipitia ripoti hiyo jana, kabla ya kuipeleka kamati ya masuala ya kimahakama leo.

Mapema jana, wakili wa Ikulu ya Marekani – White House, Pat Cipplonne alisema Ikulu hiyo haitashiriki kikao cha kamati hiyo ya masuala ya mahakama kesho, akikosoa vikali alichokiita “uchunguzi usio na msingi na unaofuata msingi wa kivyama”.

Trump mwenyewe alikemea kwa maneno makali, hatua iliyofikiwa katika uchunguzi dhidi yake.

“Na wendawazimu wale wale wanaendeleza mchakato uliochanganyikiwa, wa kunichunguza, kama mwanzo. Na wanausukuma mchakato huo, ambao ni kama kumuwinda mchawi, na mambo mabaya yanatokea upande wao. Mnaona uchunguzi wa maoni? Kila mtu anasema, haya ni bure kabisa,” alisema Trump.

Wakili Cipollone alisema katika barua aliyomtumia mwenyekiti wa kamati ya masuala ya kimahakama, Jerrod Nadler ambaye kutoka Chama cha Democrat, kwamba mchakato wa kumchunguza Trump unakiuka mifano yote ya awali, iliyokuwa na misingi ya haki.

Alisema kesho Trump atakuwa jijini London, Uingereza akihudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kujihami ya Nato.

Akijibu, Nadler alisema mwenendo wa ofisi ya Rais Trump wa kutaka kumkingia kifua, ni wenye hatari kubwa.

“Ikulu ya White House inaendekeza nadharia mpya, tena ya hatari sana. Ni mbaya kupita kinga ya jumla. Mpaka uko wapi? Ni kuzuia haki, hakuna zaidi ya hapo.

“Ikiendelea na hususan uhusikapo uchunguzi wa kamati ya kimahakama juu ya kipengele cha kumfungulia mashtaka rais, itavuruga ugawanaji wa madaraka kama ulivyowekwa na watangulizi wetu,” alisema.

Wakati mchakato huu wa uchunguzi dhidi ya Trump ukiendelea kushika kasi, kikao cha kesho kitakuwa chenye umuhimu mkubwa, kwani kitawaleta pamoja wataalamu wa masuala ya sheria, ambao ushahidi wao, pamoja na ripoti ya kamati ya masuala ya kijasusi, vitaweka msingi wa uwezekano wa kipengele cha kumshtaki rais, ambacho jopo linatarajiwa kuanza kukiandika hivi karibuni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles