29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

TRUMP AFUTA UFADHILI KWA MASHIRIKA YA UTOAJI MIMBA

WASHINGTON, MAREKANI


Donald TrumpRAIS wa Marekani, Donald Trump amesaini agizo la serikali la kuiondoa Marekani kwenye mkataba wa ushirikiano wa biashara baina ya taifa hilo na nchi 11 za Bahari ya Pasifiki (TPP).

Mpango huo unaohusisha mataifa yakiwamo Japan na  Mexico ukiondoa China, ulijadiliwa wakati wa utawala wa Rais Barack Obama lakini ulikuwa bado kupitishwa na Bunge.

Pia amezionya kampuni za Marekani kuwa zitapewa adhabu kama zitahamisha shughuli za uzalishaji nje ya Marekani.

Trump aliapa wakati wa kampeni yake kuiondoa Marekani kutoka TPP ambao alidai kuwa unawadhuru wafanyakazi wa Marekani pamoja na viwanda.

Hatua ya Trump kuiondoa Marekani katika mkataba huo haionekani kama itakuwa na athari ya haraka kwa sera za kiuchumi za Marekani, japokuwa inaashiria mtazamo mpya na tofauti wa Marekani kuhusu biashara, chini ya utawala wa Trump.

Lakini si hatua hiyo tu aliyoichukua Rais Trump katika wiki yake ya kwanza ofisini, pia amerejesha amri ya kupiga marufuku utoaji wa fedha za serikali kwa asasi za kimataifa kwa shughuli au kujadili utoaji mimba kama njia moja wapo ya uzazi wa mpango.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles