23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

TRUMP, ABE KUTAFUTA MAKUBALIANO KUHUSU KOREA KASKAZINI

FLORIDA, MAREKANI


RAIS wa Marekani, Donald Trump na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe walikutana jana katika juhudi za kutafuta msimamo wa pamoja kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.

Abe aliwasili katika eneo analopumzika Trump la Mar-a-Lago katika mji wa Palm Beach jimboni hapa kwa mazungumzo ya siku mbili, ambayo yanatarajiwa kutawaliwa na suala la Korea Kaskazini.

Lakini pia walitarajia kugusia biashara, uhusiano na China na masuala mengine.

Viongozi wote wawili huenda wakatumia mkutano huo wa kilele kujipa umaarufu wa kisiasa katika nchi zao.

Trump anakabiliwa na utata unaohusiana na uchunguzi wa Urusi kuuingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka wa 2016.

Kwa upande mwengine umaarufu wa Abe nao umepungua kwa sababu ya kashfa zinazohusishwa na visa vya upendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,244FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles