24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TRL YAANZA KUKARABATI VYOO STESHENI ZA TRENI

Na RAMADHAN HASSAN

-DODOMA

 KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL), imeanza ukarabati wa stesheni za treni ambao umezingatia uboreshaji wa mifumo ya maji, vyoo na sehemu za kukaa abiria wakati wa mvua kwa kutumia vyanzo vya ndani vya mapato.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Halima Bulembo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani, alisema stesheni ambazo tayari zimekwishakarabatiwa ni Kigoma, Kaliua, Pugu, Malindi na Mwanza, huku ukarabati katika stesheni nyingine unaendelea.

Ngonyani alisema TRL inatambua changamoto ya ukosefu wa baadhi ya huduma katika stesheni chache za reli kutokana na kuwa na miundombinu chakavu.

Alisema kutokana na hali hiyo, kampuni hiyo pamoja na serikali imeweka mpango mkakati wa kukarabati na kuboresha stesheni hizo ili kukidhi mahitaji ya sasa.

Awali, katika swali lake la msingi, Halima alitaka kujua kama serikali haioni umuhimu wa kuboresha huduma hizo ili kuwaondolea adha ya mahitaji hayo wanawake na watoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles