Trilioni mbili zatumika miradi ya kimkakati majiji sita

0
562

Amina Omari, Tanga

Serikali imetumia zaidi ya Sh trilioni mbili kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimkakati katika majiji sita nchini.

Hayo yamebainishwa na Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jaffo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo inayotelezwa na Halmashauri ya Jiji la Tanga.

Amesema kuwa miradi hiyo ina lengo la kuleta taswira mpya za kimaendeleo ikiwemo muonekano tofauti katika majiji hayo .

“Tumejenga barabara kwa kiwango cha lami na kuweka taa za barabarani, ujenzi wa madampo ya kisasa pamoja na maeneo ya kisasa ya biashara hiyo ni baadhi ya miradi ambayo inaendelea katika majiji hayo”amesema Jaffo.

Hata hivyo amewataka wakuu wa mikoa walioko katika majiji hayo kuhakikisha wanasimamia kwa ukaribu miradi hiyo iweze kuwa ni yenye viwango vyenye ubora na inayozingatia thamani halisi ya fedha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here